Uzinduzi wa ugawaji wa vitabu vya muongozo katika Halmshauri ya wilaya ya Muheza umefanyika tarehe 23/09/2022 katika ukumbi wa Comforty na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwepo wanafunzi wa shule za sekondari na msingi, Wakuu wa shule, Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe; Halima Abdallah Bulembo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Muheza Ndug; Edward Sempindu Mgaya, Afisa Elimu sekondari Ndug; Serapion Bashange, Afisa Elimu msingi Bi Pili Maximilian, Mdhibiti mkuu wa ubora wa shule Ndug; Julieth Joyce Haule pamoja na Kaimu katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Muheza (TSC) Ndug; Fatuma Rajabu.
Akizungumza katika uzinduzi huo mdhibiti ubora wa shule ndug; Julieth Haule amesema kuwa miongozo hiyo imetokana na tafiti mbalimbali za kielimu na mapitio ya udhibiti bora wa shule na maoni mbalimbali ya wadau wa Elimu, lakini pia mahitaji ya sasa kulingana na sayansi na teknolojia huku miongozo hii ikiwa inalenga hasa kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikikwamisha ubora wa elimu katika shule za msingi na sekondari.
Nae Afisa elimu Sekondari amezunguzmia miongozo ya kuwezesha elimu bora kwa wanafunzi, michakato hiyo ikiwa ni kuchakata uwezeshaji na kuboresha ufundishaji wa wanafunzi kuanzia Elimu ya awali hadi kidato cha nne, huku lengo la miongozo hiyo ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata elimu bora kwa kufaulu wote wa asilimia 100.
Aidha Mkuu wa Wilaya Mhe; Halima Bulembo ameelezea kuwa Ofisi ya Raisi TAMISEMI imeandaa vitabu vya miongozo na mikakati ya kuimarisha usimamizi wa Elimu ya msingi na Sekondari kwa lengo la kuboresha Elimu nchini, huku vikiainisha changamoto zinazoikabili sekta ya elimu, mikakati ya kuongeza ufaulu na miongozo ya kuteua viongozi wa elimu katika ngazi za shule, kata hadi Halmshauri.
Ameendelea kwa kusisitiza kuwa viongozi, wa elimu, wazazi pamoja na walimu wasimamie maadili na heshima, pia kila mwalimu aweke malengo binafsi katika masomo husika anayofundisha na kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anashindwa kupata umahiri uliokusudiwa katika somo husika, Pamoja na ushirikiano baina ya viongozi wa serikali, viongozi wa ngazi za juu za Elimu, pamoja na walimu huku viongozi wa Elimu wanajielekeza zaidi katika ufatiliaji wa ufundishaji wa walimu darasani na kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi darasani na pia kutatua changamoto zinazowakabili walimu kushindwa kutekeleza majukumu yao ya ufundishaji.
Bulembo amesema kuwa kila Afisa Elimu kuhakikisha kuwa vitabu hivyo vinagawanywa kwa viongozi wa Elimu kwenye ngazi zote za Halmshauri, na kupeleka taarifa ya utekelezaji wake kwa katibu Tawala wa Wilaya kabla ya tarehe 29 september 2022,pia viongozi wote wa Elimu kuongeza kasi ya masuala ya kusimamia Elimu katika maeneo yao wanayofanyia kazi ikiwemo pamoja na kuwasaka wanafunzi wote wenye umri wa kuanza shule basi hawakai nyumbani bali waende shuleni na kuwachukulia hatua wazazi ambao watazuia Watoto wao kwenda shule.
Bulembo ametoa rai kuwa kila eneo la utawala kushirikiana na uongozi wa shule kuandaa utaratibu wa kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wa kutwa wa shule za msingi na sekondari ili kulinda afya ya ukuaji wa wanafunzi na kuongeza umakini katika masomo yao ya kila siku.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe; Halima Abdallah Bulembo akimkabidhi kitabu cha muongozo Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Muheza Ndug; Edward Sempindu Mgaya | Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe; Halima Abdallah Bulembo akimkabidhi kitabu cha muongozo Afisa Elimu Sekondari Ndug; Serapion Bashange | Diwani wa kata ya Genge Mhe; Moses Kisiki akizungumza kwenye uzinduzi huo |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.