Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF III) awamu ya pili unajenga vyumba viwili vya madarasa, matundu sita ya vyoo, na ofisi moja ya walimu katika shule ya Sekondari Kwemkabala iliyopo kata ya Kwemkabala wilaya ya Muheza ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule hiyo,Hafla ya uzinduzi wa ujenzi huo umefanyika leo tarehe 16/9/2021 halfa hiyo imeongozwa na mratibu wa TASAF wilaya ya Muheza Bi Magdalena Kimaro akishirikiana na viongozi wengine wa kata pamoja na wakazi wa Kwemkabala , amesema serikali imetoa kiasi cha Tsh 74,331,039/= ikiwa ni pamoja na nguvu za wananchi zikihitajika ilikuweza kukamilisha ujenzi huo.
, ambapo diwani wa kata hiyo amewataka wananchi wake kujitokeza kwa wingi ili kuweza kutia nguvu kazi na kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kukamilisha ujenzi huo kwaajili ya kuwapa watoto elimu bora.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.