Ukaguzi wa ndani wa Mradi wa Tasaf katika Halmshauri ya wilaya Muheza umefanyika katika Shule ya Sekondari Kwemkabala ambapo Mradi huo ulihusisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, Ofisi moja ya walimu na Matundu sita ya vyoo. Hadi mradi huo kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi milioni 74,331,039. Ukaguzi huo ulifanywa na Mkaguzi Mkuu wa ndani Ndg, Vumilia William Saimanga, Mkaguzi Msaidizi wa Wilaya Ndg, Emmanuel Amuli, Mratibu wa Tasaf Wilaya Ndg, Magdalena Kimaro pamoja Mhasibu wa Halmshauri Ndg, Andrew Elangwa Abraham.
Katika Mradi huo vyumba viwili vya madarasa vya kufundishia pamoja na ofisi moja ya walimu vimekamilika kwa asilimia mia na vimeanza kutumika, pia matundu mawili ya vyoo vya walimu yakiwa yanatumika huku ikiwa bado havijakamilika na viko katika hatua ya umaliziaji wa uwekaji wa madirisha, Aidha matundu manne ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi yako katika hatua za mwisho za upauaji na uezekaji huku ujenzi huo ukiwa unaendelea.
Wanafunzi wakiwa ndani ya moja ya darasani kwenye moja ya madarasa yaliyoana kutumika | Majengo mawili ya madarasa shule ya sekondari Kwemkabala yaliyokamilika | Matundu manne ya vyoo vya wanafunzi yakiwa katika hatua ya kupaua | Matundu mawili ya vyoo vya walimu vimeanza kutumika huku ikiwa bado uwekaji wa madirisha |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.