Halmashauri ya Wilaya Muheza ina utaratibu wa kutoa huduma ya ugawaji kinga na dawa za magonjwa yasiyopewa kipaumbele kila Mwaka lengo likiwa ni kutokmeza magonjwa ya Minyoo, kichocho,Usubi na Matende na Mabusha.
Akitoa taarifa ya maambukizi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele wilayani humo Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Wilaya Muheza Julius Mgeni amesema hali ya Maambukizi ya Matende na Mabusha Wilayani humo imepungua hadi kufikia chini ya asilimia mbili hili ni jambo la kujipongeza kwani ugonjwa huu ulikuwa mkubwa miaka iliyopita.
Akielezea namna ugonjwa wa matende na Mabusha unavyoenezwa Mgeni amesema Ugonjwa huu huenezwa na Mbu ambao hupelekea kuvimba mikono, miguu, Titi na sehemu za siri
Katika hatua nyingine ameyataja magonjwa yatakayotolewa kingatiba awamu hii kuwa ni Kichocho, Minyoo na Usubi,ambapo Dawa na Kinga tiba za Magonjwa haya itatolewa kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili ikiwa ngazi ya jamii watapatiwa kinga tiba ngazi ya jamii tarehe 6/7/2020 hadi 10/7/2020 ambapo ngazi ya Shule Ugawaji wa Dawa kinga tiba utafanyika tarehe 26/7/2020 hadi tarehe 27/7/2020.
Aliongeza kuwa wazazi wahakikishe wanawapatia chakula cha kutosha watoto wakati wa ugawaji wa dawa na kinga tiba hizi kwani jukumu la kumuwezesha mtoto kupata chakula shuleni ni la wazazi na waachane na dhana potofu ya kuwazuia watoto wasimeze dawa hizi kwa kuzani kwamba watashindwa kupata watoto( watakuwa wagumba).
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii Wilaya Muheza Vije Mfaume Ndwanga ametoa Wito kwa Wadau kusaidia kuchangia chakula cha watoto Shuleni kipindi cha Ugawaji wa Kinga tiba hizi
Nae Mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele ngazi ya Shule ambae ni Afisa Elimu vifaa Msingi Saida Mahugu amewataka viongozi wa dini kusaidia kutoa elimu kwa waumini juu ya unywaji wa dawa wiki moja kabla ya zoezi hili.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.