Halmshauri ya Wilaya ya Muheza kupitia Mapato yake ya ndani imenunua pikipiki saba (7) zenye thamani ya shilingi Milioni kumi na saba na laki tano (17,500,000) na kuzikabidhi kwa maafisa kilimo wa kata ili kuwezesha na kuboresha shughuli za kilimo Wilayani humo.
Pikipiki hizo zimekabidhiwa kwa maafisa ugani wa kata saba za Songa, Ngomeni, Pandedarajani, Kwezitu, Misalai, Amani na Mbomole kwa awamu ya kwanza kutokana umbali mkubwa uliopo kutoka kijiji kimoja hadi kingine ili kuwarahishia maafisa kilimo kuwafikia na kuwahudumia wakulima kwa wakati
Akizungumza wakati wa makabidhiano Mbunge wa Jimbo la Muheza kupitia tiketi ya CCM Hamis Mwinjuma (MWANAFA) ambaye pia alikuwa ni mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema Pikipiki hizo zilizotolewa kwa maafisa ugani zikatunzwe na kutumiwa vyema badala yake zisitumike kwa matumizi binafsi bali zitumike kwa matumizi yaliyokusudiwa ya kuboresha na kurahisisha shughuli za kilimo katika kata hizo.
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Wilaya ya Muheza Hoyange Marika amesema lengo la Halmashauri lilikuwa ni kuwapatiwa Pikipiki Maafisa kilimo wote waliopo Wilayani Muheza ili kurahisisha shughuli za kilimo na kuongeza uzalishaji lakini kwa kuwa Wizara ina mpango wa kuwapatia pikipiki maafisa ugani Inchi nzima hivyo basi zoezi hili la utoaji pikipiki ngazi ya Wilaya litafanyika kwa awamu hii tu.
Aidha aliwataka Maafisa kilimo hao waweze kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuleta tija na maendeleo ya kilimo Wilayani humo.
Maafisa kilimo (ugani) wakiwa kwenye pikipiki walizopewa | Mbunge wa jimbo la muheza mhe. Hamisi Mwinjuma akizungumza na maafisa ugani wakati wa zoezi la ugawaji wa pikipiki | Afisa kilimo wa wilaya ya Muheza ndg, Oyange Marika akizungumza na maafisa ugani kwenye zoezi la ugawaji wa pikipiki |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.