Meneja wa kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Ndugu Kaptain Rweikiza amefanya mafunzo na Wajasiriamali wa wilaya Muheza leo tarehe 24/01/2019 katika ukumbi wa Halmashauri ili kuwajengea uwezo wa kujua umuhimu wa bima na hatimaye wajiunge katika taasisi hiyo.
Akielezea historia ya Bima Rweikiza amesema Mamlaka ya Usimamizi wa shughuli za Bima Nchini (TIRA) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa sharia ya Bima Na.10 ya mwaka 2009 na inafanya kazi chini ya Wizara ya Fedha na Mipango na inaongozwa na Kamishna wa Bima.
Pia alivitaja vipaumbele 4 vya ( TIRA) kuwa ni kuongeza uwezo wa makampuni kutoa huduma za Bima kama vile mitaji, ukwasi,mfumo na rasilimali watu, Ajira kwa vijana wazawa katika sekta ya Bima na kupanua wigo, kusogeza huduma za bima hasa vijijini na kuboresha taswira ya huduma za bima.
Rweikiza amesema madhumuni ya Mamlaka ya TIRA ni kuweka Mazingira mazuri ya ushindani , kuendeleza sekta ya bima ichangie katika uchumi , kuhakikisha soko la bima haliingiliwi na kuwepo kwa huduma nafuu zinazomlenga mteja.
Aidha ameweka bayana shughuli za mamlaka kuwa ni kusajili makampuni ya bima, madalali, mawakala, wakadiriaji hasara , kukagua na kusimamia utendaji wa watoa huduma za bima , sheria ya bima Na. 10 ya 2009, kutoa elimu ya bima kwa umma na kushughulikia malalamiko ya wadau.
Kwa upande mwingine alitoa wito kwa wajasiriamali kujiunga na bima kwani inaleta amani moyoni wakati wote, inalinda mtaji wa biashara yako na kujikinga na majanga na kurejea katika hali yako ya awali.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.