Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TASAF Taifa PAULO KIJAZI amefungua kikao kazi cha wakuu wa Idara na mafunzo ya wawezeshaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza jana tarehe 16/6/2020 katika ukumbi wa TATE PLUS uliopo katika Kitongoji cha Genge Kata ya ili kuhakiki kaya za walengwa wa mpango wa knusuru kaya maskini na utekelezaji wa kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF.
Akisoma Hotuba ya Mkurugenzi wa TASAF Kijazi amesema tathmini ya Utekelezaji wa Kipindi cha Kwanza cha Awamu ya Tatu ya TASAF inaonyesha kuwa mpango wa kunusuru Kaya Maskini umechangia kwa kiasi kufikiwa azma ya Serikali ya kupunguza umaskini nchini. Takwimu zinaonyesha kwamba utekelezaji wa Mpango kwenye Kipindi cha Kwanza umechangia kupungua umaskini wa mahitaji ya msingi kwa kaya kwa asilimia 10 na umaskini uliokithiri umepungua kwa asilimia 12 kwa kaya maskini sana nchini.
Aliongeza kuwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini umewezesha kaya za walengwa kujikita kwenye shughuli za kukuza kipato na kujiimarisha kiuchumi ikiwemo ufugaji, Uvuvi,
Kilimo na biashara ndogo ndogo ambapo vijiji/mitaa/shehia zimefikiwa kwa asilimia 70.
Aliendelea kuwa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu cha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF 111) kitatekelezwa katika Halmashauri zote 185 za Bara na Wilaya zote za Zanzibar, utekelezaji huo utafanyika kwenye vijiji/mitaa/shehia zote nchini na kujumuisha maeneo ambayo hayakupata fursa hiyo katika Kipindi cha Kwanza cha Utekelezaji wa ambacho kimekamilika. Ikiwa Kaya Milioni moja laki nne na nusu (1,450,000) zenye zaidi ya watu Milioni 7.
Katika hatua nyingine amewataka Washiriki wa Mafunzo kuzingatia tahadhali za ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virus vya Corona ikiwemo kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, kukaa umbali wa mita moja baina ya mtu na mtu, kuepuka kushikana mikono, kunawa Maji tiririka na sabuni na kuvaa barakoa
Aliendelea kuwa zoezi la uhakiki wa taarifa za walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini utafanyika kwa njia ya simu lengo ikiwa ni kuondoa taarifa za walengwa ambao hawana sifa kama vile, Viongozi, waliofariki, waliohama na wasio maskini ili kuepuka malalamiko kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Nassib MMbagga amewataka wawezeshaji wazingatie mafunzo kwani atakaefanya uzembe katika kazi zoezi hilo atawajibishwa .
“Zoezi la uhakiki wa kaya za Walengwa ni jambo la Msingi na la Kitaifa na wasimamizi ni sisi , nawaombeni ambao mpo mfahamu kwamba mnatekeleza agizo la Rais Mhe John Pombe Joseph Magufuli, kiapo mtakachokula mkakifanyie kazi : mahali ambapo huelewi uliza atakaeshindwa kufuata maelekezo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake” alisema Mkurugenzi MMBAGGA.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.