Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Taasisi ya Haki Elimu Tanzania Godfrey Boniventura amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo Vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa watoto wenye mahitaji maalum ambao ni watoto wenye ulemavu Mkali na ulemavu usio mkali kama vile vipofu, viziwi,na walemavu wa viungo ili kuhakikisha wanakabiliana na changamoto zinazojitokeza katika elimu.
Akizungumza na kamati ya watoto wenye mahitaji maalum leo tarehe 13/05/2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya Muheza wakati wa makabidhiano GODFREY amesema alihaidi kutoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni sita (6,000,000/=) lakini ameweza kuongeza hadi kufikia kiasi cha shilingi milioni sita na arobaini na nne elfu (6,044,000/=), lengo nikuwawezesha Watoto hao kufikia malengo yao katika suala zima la kielimu kwa sababu elimu ni haki ya msingi.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni Cherehani mbili, kiyoyozi (AC), kiti cha magurudumu mawili (wheelchair) viwili Smart TV Screen moja yenye uwezo wa kuunganishwa na internet ili kuweza kujifunza vipindi mbalimbali na Dishi la kisimbuzi cha Azam.
Aidha, Mkurugenzi huyo ameiomba Halmashauri kwa juhudi walizozianzisha katika kuhakikisha wanawasaidia wototo hao wenye mahitaji maalumu ili waendelee kupambana wasiweze kuishia hapo, kwani bado wanauhitaji mkubwa na amewataka wazazi kuweza kuwalinda Watoto dhidi ya vitendo vya ukatili.
“Niwaombe Halmashauri kwa juhudi mlizozianzisha msiishie hapa na tusisubiri Serikali kuu tufanye harambee ili kuweza kuwasaidia, mafanikio ya Muheza ni mafanikio ya Taifa zima.”Alisema Godfrey.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhandisi Mhe. Mwanasha Rajab Tumbo akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Mradi amesema kuwa kama malengo yalivyowekwa kwa ajili ya kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu kiwilaya kuna watoto takribani 400. Majengo yameanza kujengwa ambayo ni mabweni mawili ya wanafunzi wakike na wakiume katika Shule ya Mbaramo na Bweni moja la wavulana kwenye Shule ya Masuguru yatakapokamilika kujengwa, litaanza kujengwa Bweni la Wasichana.
Kwa upande wake Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Pili Sindaguru ameeleza kuwa kawashirikisha wadau wa kamati ya watoto wenye mahitaji maalumu kuhudhuria katika zoezi hilo na kuungana kwa pamoja ili kupokea vifaa hivyo vya kujifunzia na kufundishia kwa sababu ni watoto ambao wapo katika mazingira magumu ya kuweza kupata elimu kwa ujumla, kwa kuweza kupata vifaa hivyo itarahisisha kufikisha ujumbe kwa walengwa.
Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Haki elimu Tanzania Gogfrey Boniventura (aliyesimama) akizungumza na wadau wakamati ya watu wenye mahitaji maalumu waakati wa zoezi la kukabidhi vifaa. | Afisa elimu Msingi Wilaya Muheza Pili Sindaguru (wakwanza kulia) akishuhudia makabidhiano ya Baiskeri ya Watoto wenye mahitaji maalumu baina ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Haki Elimu Tanzania na Mkuu wa Wilaya Muheza. | Diwani wa kata ya Mbaramo Mhe. Makame Seif Abdallah akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Haki Elimu Tanzania Godfrey Boniventura kwa kuweza kutimiza ahadi ya kuwakabidhi vifaa Watoto wenye mahitaji maalumu. | Picha ya pamoja Mkuu wa Wilaya Muheza Mhandisi Mhe. Mwanasha Rajabu Tumbo(wapi kushoto),Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Haki Elimu Tanzania Godfrey Boniventura (wapili kulia),Afisa Elimu Msingi Wilaya Muheza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Masuguru na Mbaramo. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.