Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kuwasaidia watoto na vijana wenye ulemavu pamoja na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu “Support For Future Foundation” (S4F) lenye Makao yake Makuu Jijini Dar Es Salaam kupitia Mkurugenzi Mtendaji Dr Sylivia Ruambo amekabidhi kiti cha magurudumu manne (wheelchair) tarehe 12/10/2022 nyumbani kwa mtoto mwenye ulemavu Hassan Hatibu Ally mwenye umri wa miaka 16 Mkazi wa Mtaa wa Michungwani, Kata ya Genge, Wilaya ya Muheza.
Akizungumza katika mahojiano Mkurugenzi Mtendaji Dr Sylivia Ruambo amesema kuwa Msafara huu ulifanikiwa kutembelea baadhi ya watoto wenye ulemavu ili kubaini mahitaji yao ikiwemo mahitaji ya kielimu ambapo pia ilikabidhi kiti cha magurudumu manne kwa kijana mwenye ulemavu ambaye umri wa kwenda shule umepita na anamahitaji mengine kwaajili ya kufikia ndoto zake.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Dr Edward Sempindu Mgaya amewakaribisha na kushukuru Shirika hilo kwa kutambua haki za makundi maalum na ametoa wito kwa mashirika mengine yasiyo ya Kiserikali kujumuika kwa pamoja kwaajili ya kutoa msaada kwa makundi yenye uhitaji.
Pia mama wa kijana huyo Bi Mwanaidi Mhando Mwidabi ameshukuru Shirika hili kwa msaada mkubwa alioupata na kuanisha changamoto alizokuwa anazipata mfano kulazimika kupata usafiri wa umma au kumbeba mtoto huyo pindi tu anapoumwa ambavyo vyote kwa pamoja vilikuwa ni gharama na maumivu lakini kwa sasa anaweza kutumia kiti hiko chenye magurudumu manne (wheelchair) kwa ajili ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Kwa upande wa Mratibu Mradi wa Kanda ya Kaskazini Bi Zabibu Sindangu ambaye pia ni Afisa Elimu Taaluma Msingi, amewataka wananchi wote hususani wa Wilaya ya Muheza wenye ndugu,jamaa au rafiki wenye ulemavu pamoja na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu watoe taarifa kwake kupitia simu namba 0763808721 kwaajili ya kupatiwa msaada.
Mkurugenzi Mtendaji wa S4F Dr Sylivia Ruambo(kushoto) akikaribishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Dr Edward Sempindu Mgaya(kulia). | Mratibu Mradi Kanda ya Kaskazini Bi Zabibu Sindangu(kushoto),Mtoto Mlemavu,Hassan Hatibu Ally(katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa S4F Dr Sylivia Ruambo(kulia) wakimpandisha mtoto kwenye gurudumu la matairi manne na kuonyesha namna ya kulitumia. | Mama wa mtoto mlemavu,Bi Mwanaidi Mhando Mwidabi(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa S4F(katikati) na Mratibu Mradi Kanda ya Kaskazini(kulia) wakimtoa nje mtoto mwenye ulemavu,Hassan Hatibu Ally. | Mama wa mtoto mlemavu akifata mafunzo kwa vitendo ya namna ya kutumia kiti cha magurudumu manne. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.