Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Muheza ambae ni Diwani kata ya Ngomeni Mhe, Bakari Zuberi Mhando amepongeza Serikali awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kukamilisha Miradi ya maendeleo kwa wakati.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitisha Mapendekezo ya bajeti ya Mwaka wa fedha 2020/2021 kilichofanyika jana tarehe 30/1/2020 katika ukumbi wa Chama cha Walimu anzania(CWT) Bakari amesema anaishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuipatia Halmashauri ya Wilaya Muheza kiasi cha TZS Milioni 400, kwa ajili ya kukarabati kituo cha afya Mkuzi ambacho mpaka sasa kimekamilika na baadhi ya huduma zinatolewa kituoni hapo, Pia utengenezaji wa barabara ya Muheza – Amani ambayo mpaka sasa Mkandarasi yuko site.
Akiendelea kupongeza jitihada za JPM, Mwenyekiti wa Halmshauri amesema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe, ummy Mwalimu ameahidi kutoa msaada wa TZS Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Misalaii pamoja na gari la wagonjwa (Ambulance) ili kurahisisha usafiri wa wagonjwa mahututi na kupunguza idadi ya vifo wilayani humo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo amewataka waheshimiwa Madiwani kuhakikisha vigodoro havifanyiki katika kata zao kwani husababisha ongezeko la Utoro Shuleni, Uvunjifu wa Maadili katika jamii na Ongezeko la idadai ya Mimba kwa wanafunzi.
“Nawaomba kutoruhusu vigodoro katika kata zenu ili tuongeze ufaulu wa wanafunzi shuleni kwani wapo wanafunzi waliofeli kidato cha nne kwasababu hawaendi Shule wanaishia kwenye vigodoro” alisema Mwanasha.
Aidha baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Muheza limepitisha kwa kishindo Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mwaka wa fedha 2020/2021 kiasi cha TZS 27,384,156,250 ikiwa TZS 21,294,720,000 Mishahara, Matumizi mengine 1,096,900,500, miradi ya maendeleo 2,576,315,750,ambapo mapato ya ndani Tzs 2,100, 000,000, ikiwa TZS 200,000,000 ni CHF, NHIF , Tele kwa tele na 116,220,000 ni Ada ya Sekondari.
|
|
|
---|---|---|
MKUU WA WILAYA MUHEZA AKIZUNGUMZA WAKATI WA KIKAO CHA BARAZA KILICHOFANYIKA JANA TAREHE 30/1/2020 | MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA MUHEZA BW NASSIB MMBAGGA AKIZUNGUMZA KATIKA BARAZA LA MADIWANI | DIWANI KATA YA MAKOLE MHE, SHABANI ACHIMWENE AKISISITIZA JAMBO KATIKA KIKAO HICHO |
|
|
|
KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), MHE, MOHAMMED MOYO AKIZUNGUMZA WAKATI WA BARAZA HILO. | MWENYEKITI WA KAMATI YA ELIMU, AFYA NA MAJI AMBAE NI DIWANI KATA YA MAGILA MHE DAVID KILUA AKIWASILISHA TAARIFA YA KAMATI KATIKA BARAZA HILO. | DIWANI KATA YA MISOZWE MHE, JESTINA MTANGI AKIZUNGUMZA WAKATI WA BARAZA LA MADIWANI. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.