Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kwa kupata hati Safi kwa muda wa Miaka mitatu mfululizo kwa Mwaka 2016/2017 , 2017/2018 na 2018/2019 ambayo ni hatua nzuri ya maendeleo ya Wilaya hiyo.
Aliongeza kuwa unyenyekevu, busara na Ushirikiano baina ya Viongozi wa Halmashauri , Waheshimiwa Madiwani, na Mkuu wa Wilaya ndio nyenzo madhubuti zilizopelekea kupatikana kwa hati safi hiyo hivyo basi amewataka viongozi hao kuendelea kuchapakazi kwa weledi mkubwa ili kuleta maendeleo.
Ameyasema hayo tarehe 20/05/2020 katika kikao Maalum cha baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa za hesabu za Serikali (CAG) za Mwaka wa Fedha 2018/2019 kilichofanyika katika Ukumbi wa TATE PLUS uliopo katika kata ya Genge Wilayani Muheza.
Vile vile amemuagiza Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mhandisi Mwanasha Rajabu Tumbo kusimamia wataalam wote ambao wana pesa za Makusanyo ya Halmashauri Mkononi ambazo bado hawajaziwasilisha mahali husika warejeshe kabla ya tarehe 15/06/2020 na atakaye shindwa kurejesha ndani ya muda huu apelekwe mahakamani.
Aidha amewataka waheshimiwa Madiwani kutokutumia kigezo cha dini na kabila ili kujipatia nafasi katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Akitoa sababu za kutokukamilika kwa miradi miwili ya maendeleo , mradi wa maji kilapura – PONGWE- MUHEZA na Mradi wa Barabara MUHEZA- AMANI Mheshiwa Mkuu wa mkoa amesema Ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona umepelekea kufunga usafiri wa anga ikiwa wataalam wanaotekeleza miradi hii wanatoka Nje ya Nchi hivyo basi miradi hii itaanza hivi karibuni iwapo usafiri huo utakapofunguliwa .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe.Mwanasha Rajab Tumbo ameeleza kuhusuiana na kampeni kabambe ya utoaji wa elimu kwa vitendo dhidi ya kujikinga na Ugonjwa wa Corona inaendelea nyumba kwa nyumba ambapo wataalam mbalimbali wanahimiza juu ya uvaaji Barakoa na unawaji wa mikono na tahadhali nyingine za Corona.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Nassib Mmbagga ameahidi kuendelea kufuatilia na kusimamia hoja zilizobaki akiwa na lengo la kuzipunguza ili zibaki chache au kuzikamilisha kabisa.
Akizungumzia suala la utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na wenye Ulemavu Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Muheza Mhe. Mohamed Moyo ameipongeza Halmashauri na baraza la madiwani kwa kutoa mikopo hiyo kwa walengwa na kuwata kuendelea kuvipatia fedha vikundi ili kuwakwamua kiuchumi na kuendelea kukijenga chama cha mapinduzi wilayani humo.
“pongezi Wataalam Muheza na Madiwani kwa kutoa fedha za mikopo kwa kina mama na wanawake wenye Ulemavu , pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji kwa kusimamia utoaji wa mikopo”Alisema Mohamed Moyo.
|
|
|
|
|
|
---|---|---|---|---|---|
MKUU WA MKOA WA TANGA Mhe. MARTINE SHIGELA ALIPO WASILI WILAYANI MUHEZA. | MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA MUHEZA NASSIB MMBAGGA AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA KUWASILISHA TAARIFA YA HESABU ZA SERIKALI (CAG). | PICHA YA PAMOJA BAINA YA MKUU WA MKOA Mhe.MARTINE SHIGELA NA VIONGOZI WA WILAYA YA MUHEZA BAADA YA KUHITIMISHA KIKAO. | WAHESHIMIWA MADIWANI, VIONGOZI WA HALMASHAURI NA WATAALAM MBALIMBALI WAKISIKILIZA HOJA ZA KUWASILISHA TAARIFA YA HESABU ZA SERIKALI (CAG). | MKUU WA MKOA WA TANGA Mhe.MARTINE SHIGELA,MKUU WA WILAYA YA MUHEZA Mhe. MWANASHA RAJAB TUMBO PAMOJA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA (W) MUHEZA NASSIB MMBAGGA.
|
MHASIBU WA HALMASHAURI YA WILAYA MUHEZA YUSUPH AMBAKISYE JENGELA AKISOMA TAARIFA YA HOJA YA HESABU ZA SERIKALI (CAG) 2018-2019.
|
|
|||||
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela (wapili kushoto) akisalimiana na viongozi wa Wilaya Muheza mara baada alipo wasili wilayani humo huku akichukua tahadhali ya ugonjwa wa Corona. | Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Nassib Mmbagga alipokuwa akizungumza katika kikao maalum cha baraza la Madiwani wakati wakiwasilisha taarifa ya hesabu za serikali (CAG) kilicho fanyika tarehe 20/05/2020 Muheza. | Picha ya pamoja baina ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Marine Shigela na viongozi wa Wilaya ya Muheza baada ya kuhitimisha kikao maalum cha baraza la Madiwani la kuwasilisha taarifa hesaba za Serikali kilicho fanyika tarehe 20/05/2020 Muheza. | Waheshimiwa Madiwani, viongozi wa Halmashauri na Wataala mabalimbali wakiwa katika kikao maalum cha baraza la madiwani kilicho fanyika katika ukumbi wa TATE PLUS kata ya GENGE wilayani Muheza walipokuwa wakisikiliza hoja za uwasilishwaji taarifa ya hesabu za Serikali(CAG) tarehe 20/05/2020. | Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela(wa tatu kushoto), Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhe. Mwanasha Tumbo (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza (wapili kulia) wa kiwa na kamati ya Urinzi na Usalama wakiwa katika picha ya pamoja baadaa ya kuhitimisha kikao maalum cha baraza cha kuwasilisha taarifa ya hesabu za serikali mwaka 2018-2019 kilicho fanyika tarehe 20/05/2020.
|
Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Yusuph Jengela akisoma taarifa ya hoja ya uwasilishaji hesabu za serikali (CAG) ya mwaka 2018-2019 katika kikao maalum cha Madiwani kilicho fanyika tarehe 20/5/2020.
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.