Nature Tanzania ni Asasi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na uhifadhi wa Mazingira, Maendeleo ya jamii na Uhifadhi wanyamapori imetoa fedha kiasi cha shilingi Milioni kumi na moja laki saba na mia mbili hamsini (11,707,250) kwa vikundi 3 vya wakulima wa Mazao ya Viungo vyenye wanachama 33 ili kuongeza thamani na kukuza biashara ya Mazao hayo.
Hafla ya kukabidhi hundi hiyo imefanyika siku ya ijumaa Aprili 08, 2022 iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe Halima Bulembo katika kijiji cha Shebomeza kata ya Amani Wilayani Muheza.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu huyo wa Wilaya ameipongeza asasi ya Nature Tanzania kwa kuona umuhimu wa kutoa mikopo kwa wakulima hao na kusema kuwa itasaidia kuongeza mapato ya Wilaya hiyo
Pia alitoa rai kwa wakulima wa mazao ya viungo kuacha kufanya kilimo cha mazoea bali wafanye kilimo chenye tija
“Tuache kufanya kilimo cha mazoea, tufanye kilimo chenye tija tutambue kwamba kilimo cha viungo ndio kinachoiingizia mapato Halmashauri yetu kwa kiasi kikubwa, nchi nzima inatutegemea sisi tushirikiane ili tufike mbali kwa mikopo hii tunayopokea” alisema Bulembo
Awali akisoma risala kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa taasisi ya Nature Tanzania Bw. Emmanuel Mgimwa amesema mikopo hiyo imetolewa kwa vikundi 3 ambapo kikundi cha MBOMOLE hill spice farmers group kimokopeshwa Shilingi 6,142,250, ikiwa TIFANE kimepatiwa Shilingi 3,065,000 na TUMAINI AKINA MAMA kikinufaika na Shilingi 2,500,000/=.
Aliendelea kuwa dirisha la pili la awamu ya kwanza ya mikopo linatarajiwa kufunguliwa mnamo Mwezi Julai 2022 ambapo jumla ya Shilingi 12,000,000/= zitakopeshwa kwa wakulima wa mazao ya viungo ili kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya viungo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati maalum ya mikopo ambaye pia ni afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Sylvester Mziray amesema wakopaji wanapewa miezi 3 ya ya matazamio kabla ya kuanza marejesho hivyo basi anawasisitiza kulipa kwa wakati ili waweze kuongezewa mkopo pia kuweza kukopesha vikundi vingine.
Wakipongeza taasisi ya Nature Tanzania baadhi ya wanufaika wamesema wanaishukuru asasi hii kwa kuona umuhimu wa kuwaletea mkopo huu utakaosaidia kuwainua uchumi kwani.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.