Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel ameiyagiza Bohari ya Dawa (MSD) kuhakikisha zoezi la kupeleka vifaa tiba katika Hospital ya Wilaya ya Muheza iliyopewa jina la Rais wa Tanzania Samia Suhulu Hassan linakamilika ili kuwapunguzia Wananchi adha ya kupata huduma za Matibabu.
Mollel ametoa maagizo hayo jana baada ya kutembelea na Kupatiwa taarifa ya Hosptial hiyo ambayo imeonyesha licha ya kuto kukamilika kwa baadhi ya Majengo ila majengo ambayo tayari yameshakamilika yanakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba jambo ambalo Wananchi wanashindwa kupata huduma kufuatia changamoto ya vifaa tiba kutokukamilika kwajili ya kutoa huduma kwa asilimia kubwa.
"Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani ameshatoa fedha zaidi ya Milioni 400 kwajili ya kununua vifaa tiba kwenye Hospital hiyo ambapo amehaidi kufuatia kwa karibu kutambua kwanini Bohari ya Dawa hadi sasa wameshindwa ulipeleka vifaa tiba hivyo kwakuzingatia Hospital hiyo tayari imepewa jina la Rais wa Tanzania. Alisema Naibu Waziri Mollel.
Pia Naibu Waziri Mollel kwenye ziara yake hiyo alikagua ujenzi wa kituo cha Afya cha Kwafungo kilichopo Tarafa ya bwembela kituo kinacho jengwa kwakutumia fedha za tozo za Miamala ya simu kiasi cha Milioni 250
Akiwa katika eneo hilo Naibu Waziri alipokea kilio cha Wananchi juu ya upatikanaji wa Dawa ya Nyoka ambayo inachangia Wananchi wengi kupoteza Maisha kwakukosa huduma hiyo, ambapo alimuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt, Flory Kessy kuhakikisha anapoagiza Dawa ni lazima ahakikishe dawa hiyo inakuwepo ili kuwasaidia Wananchi wa Muheza.
Awali Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Muheza ambae pia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi, Desderia Haule amemuomba Naibu Waziri kusaidia Upatikanaji wa vifaa tiba kwenye hospitali hiyo kwakuzigatia Hospitali hiyo imebeba jina la Rais wa Tanzania Samia Suluh Hassani jambo ambalo limekuwa likiwatia nguvu Wananchi kuwa huduma ambazo zitakuwa zinatolewa kwenye Hospital hiyo zitakuwa ni bora zaidi.
Kwaupande wake Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamisi Mwijuma licha ya kuishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo amemuomba Naibu Waziri Mollel kuitizama Wilaya ya Muheza kwa macho ya ziada katika kuhakikisha Wahudumu kwenye Sekta ya Afya kama Mipango ya Serikali katika kutoa huduma kwa Wananchi Wake.
"Wilaya ya Muheza licha ya kuwa na vituo viwili ya Serikali vya kutolea huduma ila bado wanakabiriwa na changamoto ya watumishi hivyo Serikali inapowapanga watumishi ni vema ikaitizama Muheza". Alisema Mbunge wa muheza.
|
|
|
|
|
|
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akisalimiana na Viongozi wa Wilaya ya Muheza mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ikiwa ni ziara yake ya siku moja.
|
Sehemu ya Watumishi wa Wilaya ya Muheza na Wadau wa Maendeleo wa Muheza wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya | Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Muheza ambapo alikagua baadha ya majengo pamoja na kuzungumza na Wahudumu wa Hospitali hiyo.
|
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel aliwasili katika Kituo cha Afya cha Ubwari kwaji li ya kukagua eneo linalo ombwa na Halmashauri kwajili ya kufanyaupanuzi wa kituo hicho kutoka kwa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa(NIMR)
|
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel akipatiwa Maelezo juu ya Tafiti ambazo zinafanyika katika kukabiliana na Wadudu ambao wanaeneza Magonjwa ya binadamu katika chuo cha Afya na Sayansi shirikishi Muheza.
|
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel akikagua Ujenzi wa kituo cha Afya kinacho jengwa Tarafa ya Mbwembera wilayani muheza |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.