Naibu Waziri Nishati Subira Mgalu atembelea wilaya Muheza jana tarehe 29/3/2019 katika miradi ya umeme iliyopo katika vijiji vya Mamboleo Lusanga, Misongeni na Mamboleo Nkumba ili aweze kujiridhisha na hatimaye afungue miradi hiyo.
Akitembelea katika vijiji hivyo aliweweza kuzindua umeme katika Nyumba ya makuti ilopo katka kijiji cha Mamboleo Nkumba , Mamboleo lusanga na Msikiti wa Misongeni ,Aidha ametuma salamu kwa wale wanaoibeza jitihada za Serikali Awamu ya tano za kuwaunganishia wananchi wa vijijiniumeme pasipo kubagua aina ya makaziyao. “ Serikali haitarudi nyuma , itaendelea kuwahudumia wananchi wote bila ubaguzi” alisema Mgalu.
Akiendelea kupongeza Jitihada za Serikali awamu ya amesema imepunguza gharama za uunganishaji wa umeme kutoka TZS 177,000/ Hadi kufikia TZS 63,000/ ambapo OMETA TZS 36000, kuunganisha umeme TZS 27000 zilizosalia zinalipwa na Serikali.
Akizitaja sababu za kukatika umeme wilayani humo Subira amesema shughuli za kilimo za kuchoma mashamba zimeunguza njia ya umeme , na kusababisha nguzo 18 kuanguka , matengenezo ya njia kuu ya umeme yanayoendelea huko Ubungo jiji la Dares salaam , miundombinu chakavu aidha amewamtaka Meneja wa Kampuni ya TANESCO Wilaya kutoa taarifa kwa umma kabla ya umeme kukatika .
Kwa upande mwingine alitoa ufafanuzi wa suala la Bomba mafuta kutoka Hoima Uganda mpaka Chongoleania Tanga, Tanzania ambao umeonekana kukwama amekanusha usemi huu na kusema mazungumzo ya naendelea baina ya mawaziri wan chi nane na kusema kuwa Vijana watanufaika na mradi huo kwani watapata ajira pia wameandaa mafunzo na taasisi ya TPDC kwa ajili ya kupata ujuzi wa kazi hizo.
Naibu Waziri Nishati akitembela miradi ya REA Muheza |
|
Naibu Waziri Nishati akitembelea mradi wa ujenzi wa hospitali Wilaya Muheza |
---|---|---|
|
||
|
||
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.