MWENYEKITI TUME HURU YA TAIFA AKIKAGUA MAFUNZO KWA VITENDO
Posted on: February 7th, 2025
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele akigagua mafunzo ya vitendo ya Waandishi Wasaidizi ngazi ya Jimbo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga katika siku ya pili ya mafunzo yao ya siku mbili Februari 7,2025. Mafunzo hayo ni maandalizi ya zoezi la Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotaraji kufanyika katika mikoa ya Tanga na Pwani kuanzia Februari 13 hadi 19,2025. Mwenyekiti pia alipata fursa ya kuzungmza na washiriki hao ambapo aliwasisitiza juu ya ushirikishwaji wa wadau katika kufanikisha zoezi hilo.
Kauli mbiu
" Kujiandikisha kuwa Mpiga kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora".