Halmashauri ya Wilaya ya Muheza leo tarehe 19/5/2022 imezindua chanjo dhidi Ugonjwa wa kupooza kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 yaani watoto wenye umri wa Mwezi 0-59 uliofanyika katika kituo cha afya ubwari kilichopo katika kitongoji cha Mbaramo kata ya Mbaramo.
Hafla hii imeongozwa na Diwani wa kata ya Mbaramo Mhe, Pugae Mohammed na kuhudhuriwa na wataalam wa afya na wazazi/ walezi wa watoto wenye umri wa kupata chanjo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Pugae amesema chanjo hiyo ni salama na haina madhara yeyote hivyo basi wazazi/walezi waliofika kwa ajili ya wakawe mabalozi kwa wenzao ambao hawajafika katika tukio hilo ili kuwakinga watoto wao dhidi yaa ugonjwa wa kupooza.
Aidha amewataka wazazi au walezi hao kushiriki kikamilifu katika zoezi la sense ya watu na makazi
“wakina mama wenzangu niwaombe tusiwafiche watoto wakati wa sense ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mnamo Agosti 23, 2022 ili kuweza kuisaidia Serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa usahihi katika sekta ya Afya” alisema Mhe Pugae.
Kwa upande wake Mratibu wa Chanjo Wilaya ya Muheza Bi. Grace Mwaimu amesema kampeni hiyo ya siku nne (4) itakamilika Mei 21 Mwaka huu na lengo la Wilaya ni kufikia watoto 31,203 wenye umri chini a miaka mitano.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.