Halmashauri ya Wilaya Muheza imekabidhi pikipiki moja aina ya Boxer kwa afisa ugani wa kata ya Tongwe ili kuimarisha shughuli za ugani zilizopo katika maeneo yote ya kata ya hiyo.
Makabidhiano hayo yamefanyika baina ya afisa Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Muheza Bw. Edward Mgaya na Afisa ugani wa kata ya Tongwe Ndugu Yohana Luoga jana katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya Muheza (BOMANI) na kushuhudiwa na afisa mifugo Juma Magoma.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Afisa mifugo na Uvuvi wa Wilaya hiyo amesema pikipiki hizo zimetolewa na Serikali kwa ajili ya shughuli za ugani hivyo basi zitunzwe na zikafanye kazi kama ilivyokusudiwa.
“Piki piki hizi zimetolewa kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao yatokanayo na shughuli za mifugo hivyo ikatumike ipasavyo kuhakiksha uzalishaji huo unaongezeka zaidi kwa ajili ya kuongeza mapato ya Halmashauri na kipato cha wananchi” alisema Mgaya.
AFISA MIFUGO (W) AKABIDHI PIKIPIKI
|
AFISA MIFUGO (W) AKABIDHI PIKIPIKI
|
|
|
Afisa Mifugo na uvuvi Wilaya ya Muheza Edward Mgaya (kushoto) akikabidhi pikipiki kwa afisa ugani wa kata ya Tongwe jana katika ofisi za Halmashauriya Wilaya ya Muheza. |
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.