Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe.Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo akishirikiana na timu ya Uhamasishaji Ugonjwa wa Corona leo tarehe 25/04/2020 wametembelea katika kata sita za mjini Majengo,Masuguru,Mbaramo,Tanganyika, kwemkabala na Genge ili kutoa Elimu kwa wananchi juu ya Ugonjwa wa huo.
Katika zoezi hilo wameweza kutembelea katika maeneo mbalimbali maduka ya rejareja, saluni za kike na kiume, baa za bia bucha za nyama vituo vya waendesha pikipiki (maarufu kama bodaboda), kituo cha mabasi kilichopo kata ya Genge na nyumba za watu binafsi.
Walipotembelea katika kituo cha bodaboda kilichopo katika kitongoji cha uhuru kata ya Masuguru Mkuu wa Wilaya aliwataka waendesha vyombo ya moto hivyo kuzingatia tahadhari ya ugonjwa wa Corona ikiwemo kutopakiza abiria zaidi mmoja (mishikaki) na kuhakikisha kila mtumiaji wa Chombo hicho anakuwa na Barakoa, vitakasa mikono na wanapo kuwa kijiweni wakae umballi zaidi ya mita moja kwa mtu mmoja hadi mwingine.
Kwa upande mwingine aliwataka wazazi kuwazuia watoto ambao kwa sasa wako majumbani ili kuwakinga na mlipuko wa ugonjwa huu pamoja na ukatili wanaofanyiwa wakiwa mtaani ikiwemo ubakaji.
Nae Mganga Mkuu Wilaya Flora Kessy amewataka madereva wa Magari ya abiria kuhakikisha abiria waliomo ndani ya gari hawasimami bali wakae ‘level sit’ ili kuepuka msongamano.
Akitoa maelekezo ya unawaji mikono Afisa Afya Wilaya Abubakari Rashidi amesema zoezi hili lifanyike kwa kutumia maji tiririka na sabuni au kwa kutumia vitakasa mikono (sanitizer)
Pia ameelekeza wananchi namna ya kuvaa Barakoa (mask) kuwa unapoivaa unatakiwa kukaa nayo ndani ya masaa 4-6 hazipaswi kuvaliwa kutwa nzima na kurudia matumizi hivyo kila mtu anatakiwa kutembea na Barakoa zaidi ya moja.
Kwa upande wake mjumbe wa Timu ya hamasa ambae ni Mhandisi wa Maji Kapota Kapota amewaasa wanachi kuchukua tahadhri ya ugonjwa wa corona kwa kutowapokea wageni kutoka maeneo ndani na nje bali wawasiliane kwa simu ili kuweza kujikinga na maambukizi.
“Ndugu zangu tuepuke kupokea pokea wageni kutoka sehemu mbali mbali iwapo mtu atataka kuja kwako kipindi hichi mwambie asubiri Corona ipite sasa hivi tuwasiliane kwa njia ya simu tu” alisema Mhandisi wa maji.
MKUU WA WILAYA MUHEZA AKITOA ELIMU KITUO CHA MABASI | MKUU WA WILAYA AKIZUNGUMZA NA WAJASIRIAMALI WALIOPO KITUO CHA MABASI MUHEZA | AFISA AFYA WILAYA AKIELIMISHA UNAWAJI MIKONO | MHANDISI WA MAJI AKIZUNGUMZA NA DEREVA BODABODA. |
Mkuu wa wilaya Muheza Mhe, Mwanasha Rajab Tumbo (alieshika kipaza sauti) akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa matunda waliopo katika kituo cha mabasi. | |||
Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo akitoa elimu kwa madereva na abiria wanaotumia usafiri wa jumuiya jana katika kituo cha mabasi kilichopo katika kata ya Genge. | Afisa afya Wilaya Abubakari Rashidi akitoa elimu ya namna ya kunawa mikono kwa watumishi na wafanyabiashara | Mhandisi wa Maji kapota kapota akitoa elimu kwenye kaya na dereva bodaboda. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.