Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ni miongoni mwa Wilaya 8 na Halmashauri 11 zinazounda Mkoa wa Tanga ina Tarafa nne (4), kata 37, vijiji 126 na vitongoji 494,
Akizungumza wakati wa kikao cha baraza la Madiwani Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Nassib Mmbagga amesema katika operesheni ya uwekaji wa anwani za Makazi Halmashauri ilikisia kuandika jumla ya anwani za makazi 59790 ambapo hadi sasa Halmashauri imekusanya jumla ya anwani 58,578 ambayo ni sawa na asilimia 97.97.
Aliendelea kuwa kazi zilizofanyika mpaka kufikia hatua hiyo ni utoaji wa elimu kwa umma kuhusu mfumo wa anwani za Makazi ambapo kata zote 37 zimefikiwa, namba za anwani 58578 na barabara 1930 zimetambuliwa na kupewa majina
Aliongeza kuwa kazi zinazoendelea kufanyika mpaka sasa ni kuandaa na kusimika vibao vya namba za nyumba na nguzo zenye mbawa za majina ya barabara/mitaa ikiwa ni pamoja na kuhakiki taarifa za Anwani za makazi na kusafisha taarifa za Anwani za makazi (data cleaning)
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imepokea jumla ya Shilingi 154,999,818.59 ikiwa ni ruzuku kutoka Serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi la uwekaji anwani za makazi ambapo mpaka sasa fedha hizo zimekwishatumika kwa shughuli 2 za kuainisha na kuandika kuta au geti namba za nyumba/majengo na kukusanya taarifa za anwani za makazi.
“Niwapongeze waheshimiwa madiwani, watendaji wa kata na vijiji, wenyeviti wa vijiji, wenyeviti vitongoji, viongozi wa dini, wadau mbalimbali, vijana na wananchi wote kwa ushirikiano mliouonyesha katika zoezi hili nawasihi tuendelee kushirikiana katika mazoezi mengine” alisema Mmbagga.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.