Wilaya ya Muheza ikishirikiana na Shirika la “ROOM TO READ” wameadhisha wiki ya usomaji wa vitabu ili kuwafanya wanafunzi wa darasa la kwanza na daras la pili kuwa na mazoea na mapenzi ya kusoma vitabu kwa lengo la kuwawezesha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.
Hafla hiyo imefanyika siku ya tarehe 1/10/2021 katika Shule ya Msingi Muheza Estate iliyopo katika kitongoji cha Tanganyika Wilaya ya Muheza na kuhudhuriwa na baadhi ya wanafunzi wa shule zote za Msingi 119 zilizopo Wilayani Muheza, walimu, na mwakilishi wa “room to read” na wakuu wa idara na vitengo na wananchi.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii na Diwani kata ya Genge Mhe, Mosses kissiky amaesema ameliomba shirika la room to read lisaidie kutatua changamoto ya nyumba kwa kuwa wao ni wadau muhimu wanaosaida Serikali kutatua changamoto za miundombinu.
Awali akizungumzia lengo la maadhimisho ya wiki ya usomaji vitabu Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Muheza Bi.Pili Maximillian amesema shirika la room to read limekuwa msaada mkubwa kwa kuwa Halashauri kwa kushirikiana na shirika hilo wameweza kuboresha maktaba katika Shule 50 za Msingi.
Kwa upande wake Afisa mradi wa Shirika la “ROOM TO READ” Bi. Sabina Matonya amesema shirika hilo linajishulisha na kukuza stadi na tabia ya usomaji kwa wanafunzi wa msingi kujenga maktaba na vifaa vyake pmoja na kukusza stadi ya kusoma kwa walimu na wanafunzi.
Aidha katika maadhimisho hayo wanafunzi wa shule za msingi mbalimbali zilizopo wilayani humo walifanya mashindano ya kusoma vitabu, kukimbiza kuku, kukimbia na gunia, kukimbia na ndimu, kukimbia na chupa, na kuvuta Kamba ambapo washindi walikabidhiwa zawadi mbalimbali na mgeni rasmi.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.