Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga jana Oktoba 30,2023 imeadhimisha siku ya lishe Pamoja na uzinduzi wa programu ya lishe ya Vijana balehe ili kuwapatia elimu vijana balehe wenye umri wa kuanzia miaka 10 hadi 19 kutambua lishe bora itakayowawezesha kuongeza kiwango cha ufaulu darasani.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Uwanja wa Jitegemee yakiongozwa na kauli mbiu isemayo “Lishe bora kwa Vijana balehe, chachu ya Mafanikio yao.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Bi. Emmanuela Lawrence amesema Vijana wenye umri wa kubalehe yaani miaka 10 hadi 19 wanatakiwa kula vyakula vinavyozingatia makundi 5 ya vyakula ambayo ni vyakula vya asili ya nafaka, ndizi,za kupika na vya asili ya mizizi kama viazi, mihogo, vyakula vya jamii ya kunde, asili ya Wanyama, na mbegu za mafuta, mbogamboga , matunda, na sukari, asali na mafuta.
Akizitaja faida za lishe bora kwa Vijana balehe inayozingatia makundi hayo 5 ya vyakula afisa lishe huyo amesema huongeza utendaji wa akili na Uwezo wao kitaaluma kujifunza na ubunifu.
Aliendelea kuwa lishe bora kwa vijana balehe huwezesha ukuaji wa mwili unaostahili ambapo husaidia kuwa na urefu na uzito mzuri kwa maendeleo ya ujuaji wa kijana
Amesema huimarisha kinga ya mwili hivyo hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa na matatizo mengine ya kiafya sasa na baadae.
Aliongeza kuwa lishe bora kwa Vijana balehe hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yasiyoambukiza sasa na wakati wa utu uzima kama vile magonjwa ya Moyo, Kisukari, Shinikizo la damu, na Saratani.
Alihitimisha kuwa lishe bora kwa Vijana balehe huimarisha mwonekano wa mwili kama vile Ngozi nzuri, kujengeka vizuri kwa Misuli kwa Wavulana na umbo zuri kwa wasichana.
Katika hatua nyingine alizungumzia baadhi ya athari anazoweza kuzipata kijana balehe iwapo atashindwa kupata lishe bora ikiwa ni Pamoja na, kinga ya mwili kuwa dhaifu, mwonekano wa mwili usioridhisha kama vile kukosa misuli kwa wavulana na umbo zuri kwa wasichana, ukuaji wa mwili usioridhisha unaoweza kupelekea udumavu na uzito pungufu.
Aidha maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na utoaji elimu ya lishe kwa vijana balehe ikiwa ni Pamoja na wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari, Upimaji wa hali ya Lishe kwa Vijana balehe na Maonesho ya vyakula bora kwa Vijana balehe.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.