Mkurugenzi amteua Mtumishi Hodari wa Mfano ,
Katika kuadhimisha sikukuu ya Wafanyakazi Mei Mosi inayofanyika mei 01 kila mwaka Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Bi. Luiza Mlelwa amemteua Bi. Mariam Majiba Afisa Uvuvi kata ya Kigombe kama Mtumishi Hodari na wa mfano katika utendaji kazi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Jitegemee Muheza , Bi . Luiza amesema amevutiwa sana na utendaji kazi wa mtumishi huyo hasa katika upande wa ukusanyaji wa ushuru wa ada za leseni za uvuvi katika kata ya Kigombe. Pia ameongeza kuwa kwa kipindi cha Julai 2017 hadi Machi 2018 Mtumishi huyo ameweza kukusanya Tsh 20,231,900 ambayo ni zaidi ya asilimia 100 ya makadirio ya bajeti ya mwaka 2017/2018 katika chanzo hicho. Pia amewapongeza watumishi hodari wote walioteuliwa katika idara zao na kuwataka kuona kuwa zawadi pamoja na vyeti walivyopewa viwe chachu na motisha ya utendaji bora Zaidi.
Awali akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi Katibu wa TUKTA Wilaya amemuomba Mgeni Rasmi kutatua changamoto zinazowakabili watumishi ikiwa ni pamoja na Upatikanaji wa fedha za likizo kwa wakati, upandishwaji wa madaraja ili kuongeza ari ya kufanya kazi na kumuomba muajiri awasilishe makato ya mifuko ya jamii ili kuondoa usumbufu wakati wa kustaafu.
Aidha Mkuu wa Wilaya Mhe. Mwanasha Tumbo ambaye pia ni mgeni rasmi wa sherehe hiyo kwa namna ya pekee amewapongeza wafanyakazi hodari wote na kuwataka watumishi wote kufanya kazi zao kwa weledi, pia ametangaza rasmi kuanzisha vikao vitakavyofanyika kati yake na idara pamoja na sekta zote ili kujua changamoto na kushauriana nao katika namna bora ya kutatua changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kuwawezesha watumishi kujua stahiki zao.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.