Viongozi wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga mnao Disemba 30, 2023 wamezindua Msimu wa uvunaji wa mazao ya Viungo, iliki, karafuu, mdalasini na Pilipilimanga ili kuwasaidia wakulima kuvuna mazao yaliyokomaa yenye ubora utakaopelekea kuuza kwa bei zuri.
Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Tawala Wilaya ya Muheza Mohamedi Mfaki kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Juma Saidi Irando ambaye alikuwa mgeni katika zoezi hilo amesema kilimo cha mazao hayo kina tija sana kwa wakulima kama watazingatia vizuri taratibu na kanuni bora za kilimo hicho kwani kinaweza kuwatoa katika umaskini wa ipato hivyo kitawasidi kuongeza kipato cha kaya kitakachowawezesha kusomesha watoto.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameboresha miundombino ya Kilimo ikiwemo utoaji wa mbolea, dawa za kuua wadudu waharibifu wa mazao, amegawa pikipiki kwa maafisa ugani na vishikwambi ili kuhakikisha mkulima wa kawaida ana hudumiwa kwa karibu na anapata faida ya nguvu alizozitumia.
Amewataka madalali kuacha kuwanyonya wakulima wa mazao hayo kwani mara nyingi wamekuwa wakiwalalia katika bei za mzao hayo.
“Sisi kama Serikali hatutaki kuona mkulia ananyanyaswa katika masuala ya kilimo, tutapima ubora wa mazao haya na kupanga bei ili kuwasaidia wakulma waweze kuboresha maisha yao, mwaka huu wa 2023 ni Mwaka wa mwisho kwa wakulima kulaliwa” alisema Mfaki.
Ametoa wito kwa wakulima wajiunge kwenye vyama vya Ushirika ambavyovitawasidia wasiyumbishwe na wafanyabiashara hivyo vitawasidia kuwa na msimao wa bei.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Dkt. Jumaa Mhina amesema inasemekana Biashara ya Mazao ya Viungo kufikia Dollar Bilioni Arobaini na Tanzania ni Nchi ya Tatu kwa Uzalishaji kwani kwa sasa kilo moja ya karafuu inauzwa kuanzia shilingi 17,000/= hadi 18,000/= hivyo walime mazao hayo kwa wingi kwa kuzingatia ubora ili yaweze kuboresha maisha yao.
“Naguswa sana na mazao ya viungo na nimekuwa nikifuatiia kwa karibu juu ya mazao haya kwa kuwa yanagusa uchumi wa Muheza kwani asilimia kubwa ya mapato ya halmashauri yanategemea mazao hayo” alisema Dkt. Mhina.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza amewataka wataalam wa Kilimo waandae takwimu sahihi ya uzalishaji wa mazao ya viungo ili kuweza kujua idadi halisi ya uzalishaji wa kilimo cha Mazao hayo
Aidha hafla hiyo ya uzinduzi wa mazao ya Viungo imefanyika katika Kijiji cha Kweisaka kata ya Tongwe na kuhudhuriwa na wakulima, Wafanyabiashara,viongozi wa vyama vya ushirika, na taasisi zinazowezesha wakulima wa mazao ya viungo.
Mazao ya viungo Wilayani Muheza yanalimwa katika kata za Tongwe, Nkumba, Magila, Magoroto, Amani, Kisiwani, Mbomole, Misalai, Kwezitu na Zirai.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.