Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Dkt. Jumaa Mhina amewataka Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata na Vijiji kuzingatia Mafunzo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Ameyasema hayo wakati akifunga Mafunzo ya Siku Moja ya Wasimamizi wasaidizi ya Uchaguzi yaliyofanyika mapema leo Septemba 30, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano Shule ya Msingi ya Holy Family iliyopo katika Kata ya Genge Wilayani hapo.
Amesema watumie vyema Vitabu vya Kanuni na miongozo ya Uchaguzi ili waweze kusimamia vyema uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa.
Ameendelea kuwa, Kanuni hizo na Miongozo ndio Nyenzo muhimu katika Utekelezaji wa kazi za Uchaguzi kwani zitawasaidia kufanya kumbukumbu za rejea wakati wa Uchaguzi pia vitawasaidia kutoa ufafanuzi sahihi wa masuala yote ya mtiririko na Mchakato Mzima Uchaguzi.
Aidha amewataka Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata na Kijiji kuhakikisha wanahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi katika zoezi la Uandikishaji wa orodha ya wapiga kura linalotarajiwa kufanyika tarehe 11- 20/ 10/ 2024.
" Nataka zoezi la Uandikishaji lifikie asilimia 100% hivyo basi nenden mkahamasishe wananchi kwa kutumia njia za vikao vya vijiji na Vitongoji ili kuweza kufikia lengo hili" alisema Dkt. Jumaa.
"SERIKALI ZA MITAA SAUTI YA WANANCHI JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI"
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.