Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Halima Abdallah Bulembo amekula kiap oleo tarehe 21/6/2021 baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan siku ya jumamosi tarehe 19/6/2021.
Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo Mkuu wa Mkoa hiyo Mhe, ADAM MALIMA aliwaapisha wakuu wa Wilaya wapya 4 Mkuu wa Wilaya Muheza, Halima Bulembo, korogwe Basilla Mwanukuzi, Kalist Lazaro wa Lushoto na Mauld Hassan Sulumbu wa Wilaya ya Mkinga.
Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe, Adam Malima amewataka wakuu wa Wilaya hizo wakawe, waadilifu, wabunifu, wachapakazi, na watatuzi wa kero za wananchi ili kuendelea kudumisha Amani katika wilaya zao.
Aidha Mkoa wa Tanga una Wilaya nane, miongoni mwa wakuu wa wilaya walioteuliwa 4 ni wakuu wa Wilaya wapya na wengine 4 walioteuliwa wametoka wilaya nyingine ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Shaibu wa wilaya ya tanga, ghaibu Lingo Pangani, Siriel Mchemba Handeni na Abel Busalama wa Wilaya ya Kilindi.
MKUU WA WILAYA MUHEZA MHE. HALIMA BULEMBO (WA PILI KUSHOTO) AKILA KIAPO NA WAKUU WA WILAYA YA KOROGWE, MKINGA,NA LUSHOTO | MKUU WA WILAYA MUHEZA MHE. HALIMA BULEMBO(KUSHOTO) AKISAINI FOMU YA KIAPO MARA BAADA YA KUAPISHWA | MKUU WA WILAYA MUHEZA MHE. HALIMA BULEMBO AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MKUU WA WILAYA MKINGA MHE.HASSAN SULUMBU | MKUU WA WILAYA MUHEZA MHE. HALIMA BULEMBO(KATIKATI) AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KATIBU TAWALA WILAYA YA MUHEZA BI DESDERIA HAULE KUSHOTO NA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA BI. HAPPINESS LAIZER(KULIA). |
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.