Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Muheza Dkt. Jumaa Mhina amefunga Semina ya Mafunzo ya Siku 2 ya Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata yaliyoanza rasmi Februari 6, 2025 na Kukamilika leo Februari 7,2025.
Katika hotuba yake ya kufunga mafunzo amewataka Maafisa hao wa Wasaidizi ngazi,ya kata kwenda kuzingatia kanuni, taratibu na miongozo iliyotolewa wakati wa mafunzo ili kufanikisha zoezi hilo ipasavyo.
Vile vile amewasihi kutojihusisha na vitendo vya Ulevi katika kipindi hiki Cha Uboreshaji wa Daftari la wapiga kura ili kutekeleza vyema kazi iliyopo mbele yao.
Pia ametoa wito kwa Maafisa hao kuhakikisha wanalinda Vifaa vya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kukwepa kutoiletea hasara Serikali.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Mafunzo hayo Bw Issa Msumari amesema watakwenda kutekeleza kazi ya Uboreshaji wa Kudumu la Wapiga kura kama walivyopata Mafunzo.
Aidha Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura awamu ya kwanza litaanza rasmi Februari 13, 2025 na linatarajiwa kukamilika Februari 19, 2025.
Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo yamehusishwa Maafisa waaandikishaji wasaidizi ngazi ya kata 37 waliopo Wilayani Muheza yakiongozwa na Kaulimbiu isemayo " Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora"
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.