Halmashari ya Wilaya ya Muheza ilipokea fedha Serikali kuu kiasi cha Shilingi Milioni Mia Tano (500,000,000) amabazo ni fedha zitokanazo na tozo za miamala ya simu kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya Kwafungo kilichopo katika kata ya Kwafungo Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.
Fedha hizi zimejenga majengo matano (5) ambayo ni Jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Maabara, jengo la wazazi, jengo la upasuaji na jengo la kufulia.
Hadi kufikia sasa, Jengo la wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara yamekamilika ambapo huduma za wagonjwa wa nje zimeanza kutolewa tangu July 18,2022 na hadi kufikia Septemba 28, 2022 Jumla ya wagonjwa 492 wamepatiwa matibabu katika kituo hicho.
Kwa upande wa jengo la kutolea huduma za wazazi hadi kufikia tarehe 28/9/2022 limefikia katika hatua ya uezekaji wa bati ikiwa Jengo la Upasuaji likiwa katika hatua ya upauaji na Jengo la Kufulia
hatua ya Gebo.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.