Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imetoa fedha za mikopo kiasi cha shilingi milioni 136 katika kipindi cha mwezi April- june 2021 kwa vikundi 23 vya wanawake, Vijana na wenye ulemavu vyenye jumla ya watu 179 ikiwa ni kutekeleza takwa la kisheria kwa nia ya kuwakwamua kiuchumi.
Hafla ya kukabidhi hundi hiyo imefanyika Julai 2, 2021 iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe, Halima Abdallah Bulembo katika ukumbi wa mikutano wa walimu (CWT) uliopo katika kitongoji cha Genge, kata ya Genge Wilaya ya Muheza.
Awali akisoma taarifa ya ya utaoaji wa mikopo Afisa Maendeleo ya jamii Wilaya ya Muheza Bi. Vije Mfaume Ndwanga amesema kati ya Makundi hayo, vikundi vya wanawake 10 ambavyo vimekopeshwa Shilingi 51,500,000= Vijana vikundi 9 vikikopeshwa Shilingi 62,500,000, Sanjari na vikundi vya Wenye ulemavu 4 vikinufaika na Shilingi 22,000,000.
Kiasi hicho cha Mkopo kitarejeshwa bila riba na kinakopeshwa kwa Makundi hayo maalum ambapo wakopaji wanapewa miezi mitatu ya huruma (matazamio) kabla ya kuanza marejesho.
Kwa kipindi cha Mwaka huu wa fedha 2020/2021 halmashauri ya Muheza imekopesha Shilingi Milioni 337 kwa jumla ya vikundi 55 vyenye jumla ya wanufaika 473, wakiwemo wanawake 254, vijana 186 na wenye ulemavu 33.
Miongoni mwa makundi hayo, vikundi vya wanawake 27 vimekopeshwa Shilingi Milioni 152, vijana vikundi 21vikikopeshwa Shilingi milioni 152 na Wenye Ulemavu vikundi 7 wakinufaika na Shilingi Milioni 33.
Mikopo hii imetolewa kwa vikundi vinavyojishughulisha na miradi ya usafirishaji abiria na mizigo (bodaboda) ufugaji wa kuku, kilimo cha mbogamboga, karakana za kuchomelea, migahawa, maduka, kuosha magari(car wash), ununuzi na uuzaji wa viungo na nafaka,
Aidha kwa Mwaka huu wa fedha,,Halmashauri imetenga Shilingi Milioni 210 ambayo ni asilimia kumi (10%) ya makisio ya mapato yake ya ndani ya Shilingi Bilioni mbili na milioni mia moja (2,100,000,000) kwa ajili ya kutoa Mikopo kwa vikundi 42 vya uzalishajimali ambapo hadi kufikia Juni 30,2021 makusanyo ni Shilingi 1,973,946,633.40,hivyo basi kiasi cha shilingi Milioni 186 kilitolewa kwa vikundi 30 na kufikia lengo la asilimia 94, Vile vile kiasi cha shilingi Milioni 151 cha marejesho ya wanavikundi kimetolewa kwa vikundi 25.
|
|
|
|
|
|
|
|||||
|
|||||
|
|||||
|
|||||
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.