• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Muheza District Council
Muheza District Council

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Ugavi na Manunuzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Utalii
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa Kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya AFYA
    • Kilimo
    • Elimu
    • Ardhi
    • TEHAMA
      • Huduma
      • Mifumo
        • PLANREP
        • FFARS
        • PREM
        • Salary Slip Portal
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha

MILIONI 111 ZAKOPESHWA HALMASHAURI YA WILAYA MUHEZA

Posted on: November 27th, 2020


Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imetoa mkopo kiasi cha shilingi Milioni mia moja kumi na moja(111,000,000) kwa vikundi vya wanawake, Vijana na Wenye ulemavu ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato yake ya ndani ili kutimiza takwa la kisheria la Serikali Ya Awamu ya tano la kuwakwamua kiuchumi wananchi wa Wilaya hiyo.

Kiasi cha fedha hizi kimegawanjwa kwa makundi mbalimbali ambapo vimefanya matumizi mbalimbali, vikundi vya vijana wamenunua vyombo vya usafiri pikipiki maarufu kama boda boda ambazo watazitumia kusafirisha abiria kutoka sehemu moja kwenda nyingine, wanwake wameanzisha miradi mbalimbali kama ya ufugaji, uuzaji mazao ya viungo, ushonaji nguo, Utengenezaji wa Batiki na Sabuni.

Akizungumza na wajasiriamali, leo ijumaa tarehe 27/11/2020 katika ukumbi wa Walimu (CWT)  Mbunge wa Jimbo la Muheza ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mhe, Hamisi Mohammed Mwinjuma(MWANA FA) amesema atahakikisha anasimamia mikopo hiyo kwa karibu sana kuhakikisha wanawake wanapata asilimia 4, vikundi vijana asilimia 4 na Wenye ulemavu wanapatiwa asilimia 2 ya mikopo hiyo.

“nitahakikisha mikopo hii haitolewi kwa upendeleo, kila kundi litapata mkopo kama linavyostahili kulingana na mwongozo wa Serikali” alisisitiza Mhe Mbunge.

Aliendelea kuwa pesa watakazopewa wanavikundi wakazitumie kwa shughuli za kikundi ili waweze kutekeleza malengo na kuboresha maisha yao wasizitumie kununulia matumizi ya nyumbani kwani watashindwa kurejesha

Katika hatua nyingine ameahidi kuweka mikakati ya kuongeza mapato ili kiwango cha mikopo kiweze kuongezeka na kusaidia wananchi wengi kwa wakati mmoja pia atahakikisha fedha hazirudishwi kwenye Halmashauri.

Awali akisoma taarifa ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu kwa kipindi cha mwezi julai hadi Novemba 2020 Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Muheza Vije Mfaume Ndwanga amesema katika kipindi hiki Halmashauri imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Milioni mia moja kumi na moja(111,000,000) kwa vikundi 18 ikiwemo vya wanawake 10, vijana 7 na Wenye ulemavu 1.

Aliendelea kuwa vikundi hivyo vina jumla ya watu 175, wakiwemo wanawake 100, vijana 70, na watu wenye ulemavu 5 ambapo miongoni mwao wanaume wanne (4) na Mwanamke mmoja(1).

Aliongeza kuwa kwa kipindi cha mwaka 2020/2021 Halmashauri imetenga Shilingi 210,000,000/=ikiwa ni asilimia kumi ya makisio ya mapato ya ndani ambayo ni Shilingi 2,100,000,000 yenye lengo la kutoa mikopo kwa vikundi 42 vya uzalishaji mali vya wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.

Nae Mkuu wa Usalama barabarani wa Wilaya ya Muheza Ndugu Richard Mmuwe amewataka vijana wa waendesha pikipiki (bodaboda) kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali zinazoweza kuwavunja viungo vyao vya mwili, pamoja na faini na adhabu zilizowekwa kwa mamlaka Serikali. Pia amewataka wajiepushe na pombe kwani ndio inayowapelekea kupata ajali.

Kwa upande wa wanufaika wa mikopo wametoa shukrani kwa Serikali awamu ya tano inayoongozwa na DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, Mkuu wa Wilaya Muheza na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza kwa kuwaona na kuwapatia mikopo itakayowasaidia kuboresha maisha yao na kuahidi kurejesha mkopo kwa wakati.

Mbunge wa jimbo la Muheza Hamisi Mohammed Mwinjuma(MWANA FA) akizungumza kabla ya makabidhiano ya pikipiki yaliyofanyika leo ijumaa tarehe 27/11/2020 katika ukumbi wa CWT wilayani Muheza Afisa maendeleo ya jamii Wilaya Muheza Vije Mfaume Ndwanga akizungumza kabla ya kukabidhi bodaboda za vikundi.















Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI June 24, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI, VIBARUA WAKUSANYAJI USHURU June 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI, NAFASI ZA WATENDAJI WA VIJIJI, MADEREVA NA MWANDISHI MWENDESHA OFISI October 01, 2024
  • TANGAZO LA NYONGEZA KUITWA KWENYE USAILI October 03, 2024
  • Angalia Vyote

Habari mpya

  • RAIS SAMIA AKOSHWA NA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI MAGILA AMRUHUSU AKAE KWENYE KITI CHAKE CHA RAIS

    February 28, 2025
  • MICHAEL MSECHU AONGOZA WANANCHI WA MUHEZA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA

    February 19, 2025
  • WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII KUWAFIKIA WANANCHI VIJIJINI

    February 14, 2025
  • OMBI KUPATIWA HALMASHAURI YA PILI NDANI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA

    February 06, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Mhe. Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania akizindua uchangiaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sheria Ndogo za Halmashauri
  • Ratiba ya vikao vya kisheria
  • Video za Matukio Mbalimbali
  • Huduma za Afya zinazopatikana
  • Mpango Kazi wa Halmashauri
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani na Taarifa za Kata
  • Mawasiliano ya Walimu wakuu wa Shule za Msingi na sekondari

Viunganishi linganifu

  • Ikulu
  • Mbinu mbalimbali za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi , Milma ya Usambara Mashariki, Muheza.
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Idara kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Muheza Mjini, Bomani

    Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA

    Simu: 027-2977545

    Simu ya Mkononi: 0746525653

    Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.