Mbunge wa Jimbo la Muheza na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamisi Mwinjuma almaarufu (MwanaFA ) amesema ameahidi kutatua kero za watoto wenye Uhitaji maalum ikiwemo kuboresha miundombinu rafiki katika Shule zao.
Kauli hiyo ameitoa jana Jumamosi Septemba 28 alipokuwa Mgeni rasmi katika hafla ya Chakula cha Pamoja na watoto wenye Mahitaji Maalum iliyofanyika katika Ukumbi wa "Comfort" uliopo katika kata ya Mbaramo Wilayani humo.
Amesema kuwa Serikali itaendelea kuboresha Miundombinu rafiki ya watoto wenye mahitaji Maalum ili waweze kufikia ndoto zao kama ilivyo kwa watoto wengine kwani Watoto wote wana haki ya kupata elimu stahiki .
Ameendelea kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuboresha mazingira wanayoishi watoto hawa kwa kuwajengea Uzio ili kuhakikisha wanasoma katika mazingira salama.
Pia ameahidi kuwapatia Vifaa vya Michezo watoto wenye Mahitaji Maalum siku ya Jumatatu tarehe 30/9/2024 wakati wa tukio la Uzinduzi wa Kampeni ya " Mtoto wa leo, Samia wa Kesho " utakaoongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri Mkuu Mhe. Dotto Biteko (MB).
"Nawapongeza walimu, wazazi na walezi kwa kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalum, mimi kama mwakilishi wenu nitaendelea kuikumbusha serikali kuhakikisha inaendelea kujenga Majengo yenye mazingira ya watoto wenye mahitaji maalum" alisema Mbunge huyo wa Jimbo la Muheza.
Aliendelea kufafanua kuwa Serikali itaendelea kugharamia elimu Kwa kuwalipia ada watoto kuanzia chekekea kama inavyofanya.
Hata hivyo Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mwezi amekuwa akilipa kiasi cha shilingi Bilioni 1.3 kugharamia elimu mkoa wa Tanga.
Hivyo, tunaposema elimu bure si kweli bali Mheshimiwa Rais analeta pesa ambapo Ili kumuondolea ada anayotakiwa kulipa mzazi.
Aidha amekabidhi vifaa vya Shule kama vile Madaftari, kalamu, Rula kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kupunguza changamoto za kielimu zinazowakumba watoto hao.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.