Wizara ya elimu na Mafunzo ya ufundi kupitia mradi wa kusimamia stadi za KKK au “LANES” imeipatia Halmsahauri ya Wilaya ya Muheza pikipiki 33 kwaajili ya kuwawezesha Waratibu Elimu Kata katika zoezi zima la kufuatilia utendaji kazi mashuleni .Hivyo kuimarika utendaji kazi shuleni kutasaidia kuongeza ufaulu na kiwango cha taaluma. Kwa mwaka 2017 ufaulu wa wilaya ulikua 67% hivyo kwa kupatikana kwa vitendea kazi hivyo ni matumaini ya wilaya kuwa ufaulu utaongezeka
Akikabidhi pikipiki hizo leo tarehe 28/7/2018 katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Mhe Balozi Adadi Rajab aliwaasa Waratibu Elimu Kata kuwa wazitumie kama Serikali ya awamu ya Tano inavyo kusudia kuongeza ufaulu na si kwenda kuzipaki kwenye vilabu vya pombe ,amewahimiza wachape kazi kwani Serikali ipo na itawafualitila kuona matokea chanya yanapatikana kwa wana Muheza na wananchi kwa ujumla.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.