Mbunge wa Jimbo la Muheza Mkoani Tanga Mhe, Hamisi Mwinjuma amewaomba Wananchi waliopatiwa Mkopo wa Milioni 200 kuhakikisha wanatekeleza malengo ambayo wameombea Mkopo na sio kwenda kugawana.
Mbunge huyo aliyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kukabidhi Mkopo kwa vikundi 24 vya Uzalishaji Mali vya Wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu ikiwa ni fedha za Asilimia kumi ya Mapato ya ndani ya Halmashauri.
"kama Wanufaika wa leo wakishindwa kuifanyia kazi fedha ambazo wanakabidhiwa kushindwa kufanya marejesho ya vikundi na madhara yake vikundi vingine kukosa Mkopo au kujakupata fedha kidogo," Alisema Mbunge wamuheza.
Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza Erasto Mhina alisema wanatekeleza Sera ya Chama cha Mapinduzi na Maagizo ya Mhe, Rais Samia Suluh Hassani ya kuhakikisha Wananchi wanapatiwa Mikopo lengo la Serikali kuona Wananchi wanakuwa naMaendeleo kupitia fedha hizo.
"Baraza la Madiwani wataendelea kuhakikisha fedha za asilimia 10% zinakwenda kwa walengwa ambao ni Wananchi wakati walipokuwa wakiomba ridhaa kwa Wananchi moja ya ahadi ni kuhakikisha wanapata Mikopo kutoka Halmashauri ambayo haina riba kwalengo la kuwainua Wananchi wa muheza" Alisema Erasto
Kwa upande wao Wananchi ambao Wamepatiwa Mkopo huo Emanuel Konstantin ambae ni Katibu waTongwe Youth's Group na Hilda Mlopa wa kikundi cha Majengo Shimoni wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kitendo cha kuwapatia Mkopo huo ambao unakwenda kuboresha Maisha yao kwa kukuza uchumi kupitia fedha hizo.
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.