Mbunge wa jimbo la Muheza Adadi Rajab ametoa shukrani kwa viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa ukamilishaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha uongozi wake wa miaka 5 kuanzia 2015 - 2020.
Akitoa shukrani kwa Waheshimiwa Madiwani, mkurugenzi, mtendaji, Wakuu wa Idara na Watumishi wote Adadi amesema anawashukuru kwa ushirikiano mzuri waliouonyesha kuhakikisha mabadiliko makubwa ya ongezeko la miradi ya maji, vituo vya Afya, umeme na miundombinu ya barabara Wilayani humo ambapo hapo awali kabla ya uongozi wake havikuwepo.
Aliyasema hayo katika kikao cha baraza maalum la madiwani kilichofanyika mnamo siku ya jumanne tarehe 9/6/2020 katika ukumbi wa Tate plus uliopo katika kitongoji cha Genge kata ya Genge Wilayani Muheza.
akizungumzia kuhusu suala la upatikanaji wa Umeme Wilayani muheza Mhe Adadi amesema ifikapo JULY 2020 vitongoji vyote visivyokuwa na umeme vitkuwa vimepatiwa umeme.
Akielezea kuhusu Mradi mkubwa wa maji PONGWE - MUHEZA uliopo katika kata ya Mlingano Adadi amesema mpaka sasa mradi huo uko katika hatua ya mwisho ya usambazaji maji kwa wananchi ifikapo jioni ya tarehe 9/6/2020 maji yataanza kusambazwa Muheza mjini.
Aidha amewataka waheshimiwa Madiwani kuchukua fomu za maombi ya kugombea tena nafasi zao kayika uchaguzi Mkuu wa Mwaka kwa kuwa wamefanya kazi nzuri katika kipindi chao chote walipokuwa madarakani.
"Mna kila sababu inayowafanya mrudi kwenye kata zenu ili mje mtekeleze mlichoacha, kuwa na nguvu, jiamini utarudi , wale wazee wanaostaafu tunawatakia kila la kheri, ukiona una kila sababu ya kuomba chukua fomu ukiona una wasiwasi acha kuchukua fomu,, usisubiri kutolewa kwa aibu" alisema Mhe Mbunge.
kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Nassib MMbagga ametoa taarifa ya mapokezi ya fedha kiasi cha shilingi Milioni 210 kwa ajili ya umaliziaji wa vyumba vya maabara vya Shule za Sekondari ambapo zitapelekwa katika shule za Sekondari 7 ambazo ziko katika hatua nzuri ya umaliziaji kila shule itapewa kiasi cha shilingi Milioni 30.
Pia alitoa taarifa ya mapokezi ya gari ya wagonjwa ( AMBULANCE) iliyotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha Afya Mkuzi ambapo ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na DKT JOHN POMBE MAGUFULI kwa msaada huo.
Akijibu swali linalohusu ni lini ujenzi wa kituo cha Afya Mlesa kilichopo katika kijiji cha MLESA kata ya AMANI kitajengwa Mkurugenzi Mtendaji amesema kwa kuwa eneo la ujenzi wa kituo hicho limepatikana Mganga Mkuu Wilaya na timu yake ya wataalam wakakague eneo hilo ili ujenzi uanze haraka ambapo fedha za mapato ya ndani zitatumika kuanza ujenzi huo.
Vile vile alitoa taarifa ya kuanza kutoa huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya iliyopo katika kijiji cha Tanganyika Kata ya Lusanga kuwa kuanzia siku ya jumatatu tarehe 8/6/2020 huduma ya wagonjwa wa Nje ilianza kutolewa na huduma nyingine za Maabara na huduma za Afya ya Uzazi zinatarajiwa kuanza kutolewa Mnamo Mwezi July 2020.
|
|
|
|
|
|
SEHEMU YA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA MUHEZA WAKIWA KATIKA BARAZA . | MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA(W) MUHEZA NASSIB MMBAGGA AKIZUNGUMZA WAKATI WA BARAZA. | MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA MUHEZA (ALIESIMAMA) MHE, BAKARI ZUBERI MHANDO AKIZUNGUMZA WAKATI WA BARAZA HILO. | |||
WAHESHIMIWA MADIWANI WAKIWA KATIKA SALA YA PAMOJA YA KUOMBEA BARAZA KABLA YA KUANZA KIKAO | MBUNGE WA JIMBO LA MUHEZA MHE, ADADI RAJAB (KUSHOTO) AKITETA JAMBO NA MHE DIWANI KATA YA NKUMBA MHE, CHARLES MHILU MARA KABLA YA KIKAO CHA BARAZA KUANZA. | MWENYEKITI WA HALMASHAURI MHE, BAKARI MHANDO (KULIA) AKITETA JAMBO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI NASSIB MMBAGGA KABLA YA KUANZA KWA KIKAO. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.