Uzembe wa Watendaji na uzalishaji mdogo wa Umeme katika Vituo vya kuzalishia Umeme ni miongoni mwa sababu zilizotajwa kusababisha kukatia katika kwa Umeme Nchini na hii imetokana na baadhi ya Mikataba iliyoingiwa kipindi hicho cha nyuma kutokuwa na tija ya Muda mrefu.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu NEC, Itikadi , Uenezi na Mafunzo CCM Taifa Mhe Paul Christian Makonda Wilayani Muheza alipokuwa katika Ziara yake ya kusikiliza na kutatua Kero za Wananchi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Amesema wananchi waendelee kumvumilia na kumshika Mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu ambae anaendelea kuambana katika masuala mbalimbali ya Maendeleo liiwemo hili la Nishati ya Umeme ambapo mpaka sasa hatua mbalimbali zimeshaanza kuchukuliwa ili kuboresha huduma hii ikiwemo kuwawajibisha watendaji wazembe na Uboreshaji wa miundombinu ya Nishati hiyo.
“Ndugu zangu wananchi naomba mtusamehe na muendelee kumuamini Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani mpaka sasa anaendelea kupambana ambapo jitihada mbalimbai za kuboresha njia za kusafirisha umeme zinafanyika, njia za kupooza Umeme zinzfanyiwa kazi ili Umeme uweze kusambazwa kwa Wananchi” alisema Makonda.
Aliendelea kuwa Serikali imeanzisha Mradi wa kuongeza Uzalishaji wa Umeme kufikia Megawati 2500 ambao ndio Mkombozi wa Taifa ambapo mpaka sasa kiasi cha Shilingi Trilioni Sita (6) zimekwishalipwa ambapo mradi huu unatarajiwa kuwa na Vinu 8 hivyo ukamilishaji wa mradi huu utaifanya Tanzania kuwa ya Kwanza kuwa na Miundombinu bora ya Umeme na itapelekea gharama za” unit” za Umeme kupungua bei.
MAKONDA AWASILI MUHEZA |
|
|
|
|
|
||
Katibu NEC, itikadi, uenezi na Mafunzo CCM Mhe. Paul Christian Makonda leo jumapili tarehe 21/1/2024 amefanya ziara ya Siku moja Wilayani Muheza kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.