Jumla ya Makarani 1,020 wapatiwa Mafunzo ya siku 19 ya Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mnamo Agosti 23, 2022 baada ya kufaulu usaili uliofanyika katika kata zao.
Mafunzo hayo yalianza Wilayani Muheza katika tarafa zake zote 4 ambazo ni Amani, Muheza, Bwembwera na Ngomeni kuanzia tarehe 31/7/2022 na yakitarajiwa kukamilika tarehe 18/8/2022.
Katika tarafa ya Amani, mafunzo yanafanyika Shule ya Msingi Amani yakiwa na makarani 161 Ngomeni ikiwa na Makaran 234 wakiwa katika chuo cha utafiti Malti Mlingano, Bwembwera Makarani 242 wakinolewa katika Shule ya Sekondari Songa na Ukumbi wa Mikutano TARECU wakifundwa makarani 383. wa tarafa ya Muheza.
Aidha miongoni mwa Makarani hao kuna Wasimamizi wa Maudhui 89 na Wasimamizi wa TEHAMA 37 ambao pia watapatiwa mafunzo katika kipindi hicho.
Akitembelea vituo hivyo vya Mafunzo, Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Halima Abdallah Bulembo amewataka makarani wote kuzingatia mafunzo ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na weledi mkubwa.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.