Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mhe. Nassib Mmbaga katika kikao cha Baraza Robo ya Kwanza kilichofanyika tarehe 31/10/2019, amewaomba Madiwani kuwaelimisha wananchi umuhimu wa vyuo vya ufundi, kutokana na kuwepo kwa ongezeko la watoto wa mitaani. Vyuo hivi vitapokea watoto walioshindwa kufikisha alama za ufaulu wa darasa la saba.
Mhe. David Kilua Diwani Kata ya Magira alipokuwa akiwasilisha taarifa ya elimu, afya na maji ameiomba Halmashauri kuwapa kipaumbele watoto wa Muheza katika vyuo hivi vya ufundi(Mkuzi na Tongwe). Pia Jestina Mtangi Diwani kata ya Misozwe ameiomba Halmashauri kutatua changamoto ya kusimama kwa Mradi wa umwagiliaji. Ukosefu wa fedha kwaajili ya kumalizia Mradi umepelekea Mradi kusuasua hali inayopelekea wakulima kufanya shughuli zao za kilimo katika mazingira magumu, Mhe. Jestina Mtangi ameiomba kamati na wataalam kwenda Moshi zone kuwaeleza changamoto zao ili ziweze kutatuliwa kwani Mradi huu wa umwagiliaji utasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wa Muheza.
Kadhalika Mwenyekiti wa Baraza Mhe Mhando ameipongeza kamati ya UKIMWI kwa kujitaidi kuhakikisha wamepunguza maambukizi mapya ya UKIMWI mpaka kufikia 2.9% kutoka asilimia 3.1% wakati mjumbe kamati ya UKIMWI Diwani Mwanaisha Mhilu alipokuwa akiwasilisha taarifa.Vilevile Mkuu wa Wilaya Mhe mwanasha Tumbo amewakumbusha kamati kuhakikisha Miradi yote inakamilika kabla ya tarehe 30/11/2019 kulingana na makubaliano.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.