Mabadiliko ya tabia ya nchi ni mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na shughuli za binadamu kama vile uchomaji wa misitu, ukataji miti ovyo, ambayo yanaweza kuleta athari katika kilimo hivyo basi kupelekea uzalishaji mdogo wa mazao.
Mkutano wa wadau mbalimbali uliongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Mh. Erasto Mhina lengo ikiwa ni kuanzisha jukwaa la kilimo himilivu dhidi ya mabadiliko mbalimbali ya tabia ya nchi uliofanyika leo tarehe 9/9/2021 katika ukumbi wa Tate Plus Muheza Tanga,
Akizungumza na wadau katika mkutano huo Mhina alisema kutokana na kilimo cha mazoea uwanzishaji wa jukwaa hili utasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya kilimo katika wilaya yetu, ili kupata kilimo chenye tija.
Alisema kuwa mkakati wa taifa wa mabadiliko ya tabia ya nchi Tanzania umeainisha sekta ya kilimo ndio iliyoathirika zaidi hivyo uwaanzishwaji wa jukwaa hilo wilayani Muheza utasaidia kwa kiasi kikubwa namna ya kukabiliana na changamoto hizo.
Kwa upande wake Mratibu wa jukwaa la wadau wa kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabia ya nchi, Bi.Shakwaanande Natai aliweza kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu jukwaa la kilimo himilivu ambalo litaweza kuinua kilimo chenye manufaa na endelevu kitakacho weza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, aliweza kufafanua changamoto mbalimbali zitakazoweza kuwa kikwazo katika jukwaa na njia ambazo wanaweza kuzitumia ilikukabilia na changamoto hizo hivyo aliwataka wadau kuwa na ushirikano.
Awali akifafanua kuhusu hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi wilayani Muheza Kaimu afisa kilimo wilaya ya Muheza Sylvester Mziray amesema wilaya ya Muheza Mkoani Tanga inakabiliwa na athari mbaya zamabadiliko ya tabia ya nchi ambayo hali inazorotesha juhudi za Halmashauri hiyo katika sekta ya kilimo.
Aidha wadau waliweza kuchagua viongozi watano katika ngazi ya mwenyekiti, mwenyekiti msaidizi, katibu, na msaidizi wake pamoja na nafasi ya mtunza fedha ambao ndio watakao ongoza jukwaa hilo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.