Maafisa kilimo wa kata na vijiji vinavyolima mazao ya viungo wametakiwa kuzingatia mafunzo juu ya namna ya kutokomeza ugonjwa wa mnyauko wa mazao ya viungo yaliyotolewa na kampuni ya inayojishughulisha na utengenezaji na usambazaji na usambazaji wa dawa za mimea (real IPM) iliyopo Arusha ili kuweza kutokomeza tatizo hilo.
Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika jana tarehe 13/7/2021 katika Ukumbi wa TATE PLUS Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Muheza ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika semina hiyo Mhe, Erasto Jerome Mhina amesema ugonjwa wa mnyauko umemfanya mkulima asione umuhimu wa zao hilo hivyo basi wasikilize kwa makini ili wakawaelimishe wakulima waondokane na changamoto hiyo.
“Niwaombe sana sana maafisa ugani mzingatie kwa makini mafunzo ili badae tupate matokeo chanya yatakayosaidia kuongeza uchumi wa wananchi wa Muheza, utaboreshwa huduma za wananchi na kuongeza kipato na thamani ya zao hili” alisema Mhe Erasto.
Akitoa historia ya tatizo la Mnyauko wa mazao ya viungo, Afisa kilimo Wilaya Muheza Hoyange Malika Mbwambo amesema tatizo hilo lilianza mnamo mwaka 2019 katika kata 12 za Potwe, Bwembwera, Magila, Magoroto, Nkumba, Tongwe, Kisiwani, Amani Misalai, Mbomole, zirai na Kwezitu zinazolima mazao hayo ya iriki, Pilipilimanga na karafuu ambapo tatizo hili limeamethiri uzalishaji kwa asilimia 30.
Aliongeza kuwa mazao haya yanashika nafasi ya pili kati ya mazao ya biashara yanayolimwa Wilayani humo na yanaipatiwa Halmashauri takribani kiasi cha Shilingi Milioni 200 kila Mwaka hivyo basi uwepo wa ugonjwa huu umeathiri makusanyo ya mapato ya Wilaya hiyo.
“ninaamini kabisa iwapo mafunzo haya yatazingatiwa na maafisa ugani wetu yatasaidia kuzuia mnyauko na tukifanikiwa kufanya vizuri tutainua uchumi wa wakulima na Halmashauri kwa ujumla” alisema Bw. Mbwambo.
Nae Mwakilishi wa kampuni ya real IPM Gigeon William Ringo amesema wametoa dawa ya telekondema na movelia itakayosaidia kupambana na mnyauko hivyo basi maafisa ugani wazingatie Maelekezo ya dawa hizo ili wakulima waweze kuuza mazao yao nje ya Nchi.
Kwa upande wake afisa kilimo kata ya Mbomole Steven Didas amesema kuwa wamezingatia mafunzo hayo na kuahidi kutoa elimu elekezi kwa wakulima ili kuweza kutokomeza changamoto ya mnyauko wa mazao hayo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.