Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila mwaka mnamo tarehe 8 machi, kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya Muheza sherehe hizi zimefanyika leo tarehe 8/3/2019 katika kijiji cha Mbaramo kata ya Mbaramo chini ya kauli mbiu ya mwaka huu isemayo “Badili fikira kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu” ambapo wananchi walishiriki katika ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa kumwaga zege la msingi katika bweni la wavulana.
Ili kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu isemayo “badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu kaimu mkuu wa Wilaya Muheza ndugu Habibu Sempindu ameitaka jamii kubadili fikra zilizojenge zilizokuwa zikimgandamiza mwanamke kwa kuwataka washiriki kwenye midahalo, maadhimisho , na mikutano na waandishi wa habari ili wapate elimu itakayowasaidia kuzitambua hakizao kisheria, kuwaimarisha wanawake kiuchumi ili kuondokana naumaskini kwa kuwapatia mikopo.
Nae kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Bw. Godhelp RINGO ameewaasa wanawake kusimama imara na kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kujiongezea kipato kwa ajili ya maendeleo ya familia zao.
WANANCHI WA MUHEZA WAKISAIDIANA KUMWAGA ZEGE |
|
|
---|---|---|
|
||
Kaimu mkurugenzi muheza Godhelp Ringo kushoto akimkabidhi kalai la zege Afisa Vijana Wilaya Ndugu John kwingwa leo katika maadhimisho ya siku wanawake duniani yaliyofanyika katika shule ya msingi Mbaramo. |
|
Kaimu Mkuu wa Wilaya Muheza Habibu Sempindu (afisa tarafa muheza) akisoma taarifa ya maadhimisho ya wanawake duniani leo tarehe 8/3/2019 katika Shule ya Msingi Mbaramo |
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.