Maadhimisho ya siku ya Kusoma, Kundika, Kuhesabu (KKK) katika Wilaya ya Muheza yamefanyika katika shule ya msingi Muheza Estate na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Elimu ikiwemo walimu wa shule, maafisa Elimu kata, Naibu Afisa Elimu wa Wilaya Ndug; Beatus Mtumbuka pamoja na mgeni rasmi Ndug; Hobokela Wilson Afisa uhusiano wa Bank ya NMB Muheza, kushirikisha baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi zilizopo Wilayani na kuwa na mashindano mbalimbali kwa wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na mashindano ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu, mashindano ya Kukimbia, ngoma, ngonjera pamoja na mashairi.
Mashindano ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu yameshirikisha wanafunzi 15 kutoka katika shule 15 ambazo ni Kibanda, Mlingano, Nkumba Kisiwani, Mashewa, Muheza Estate, Kicheba, Mbaramo, Majengo, Jimbandeni, Mgambo, Makole, Mkulimilo, Matombo, Misalai pamoja na Mikwinini. Huku mshindi katika mashindano hayo ya Kusoma akiwa alikuwa ni Monika Amani mwanafunzi wa darasa la pili kutoka katika shule ya Msingi Muheza Estate, nafasi ya pili ikishikiliwa na Glory Philipo mwanafunzi kutoka katika shule ya msingi Nkumba Kisiwani, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Ibrahimu Selemani mwanafunzi kutoka katika shule ya msingi Mlingano.
Aidha kaimu Afisa Elimu wa Wilaya Ndug; Beatus Mtumbuka amesema kuwa Halmshauri ya Wilaya ya Muheza imeandaa shule mbili za msingi ambazo zitawakilisha Wilaya ya Muheza na mkoa kwa ujumla katika mashindano mbalimbali ambazo ni Shule ya Msingi Ubembe na Shule ya Msingi Kwemsala huku akiwasisitizia walimu wakuu wa shule hizo wawaandae wanafunzi wao.
Nae Afisa Mahusiano wa Bank ya NMB Muheza amewapongeza walimu wote kwa kufanya kazi zao vizuri za kufundisha pamoja nawanafunzi wote walioshiriki katika maadhimisho hayo, huku akihimiza wanafunzi kujifunza kwa bidii shuleni pamoja na nyumbani.
Monika Amani Mshindi wa kwanza kwenye mashindano ya kusoma mwanafunzi kutoka katika shule ya Msingi Muheza Estate alitumia sekunde 36 kusoma maneno 50 akipokea zawadi ya shilingi 20,000 | Glory Philipo Mshindi wa pili kwenye mashindano ya kusoma mwanafunzi kutoka katika shule ya msingi Nkumba Kisiwani alitumia sekunde 40 kusoma meneno 50, akipokea zawadi ya shilingi 15,000 | Ibrahimu Selemani mshindi wa tatu kwenye mashindano ya kusoma, mwanafunzi kutoka katika shule ya Msingi Mlingano, Alitumia sekunde 40 kusoma maneno 49, akipokea zawadiya shilingi 10,000 | Hoboeka Wilson, Afisa Uhusiano wa Bank ya NMB Muheza akizungumza kwenye maadhimisho ya KKK | Beatus Mtumbuka, Naibu Afisa Elimu wa Halmsahuri ya Wilaya ya Muheza akizungumza kwenye maadhimisho ya KKK |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.