Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Daniel Godfrey Chongolo amefanya ziara ya siku moja Wilayani Muheza mnamo siku ya Alhamisi tarehe 11/8/2022.
Lengo la Ziara yake ni kuona namna Wilaya hiyo ilivyotekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika shughuli mbalimbali za kiserikali hususani Miradi ya Maendeleo na kutembelea uongozi wa Chama ya cha Mapinduzi (CCM) pamoja na idara mabalimbali za Halmashauri.
Akitembelea katika Shule Mpya ya Sekondari Kisiwani iliyopo katika kata ya Kisiwa tarafa ya Amani ambayo katika ilipokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 470 (470,000,000) kutoka Serikali kuu kupitia Mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP) ambayo mpaka sasa ipo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji Chongolo amesema Shule hiyo iko katika mazingira rafiki ya kujisomea anakwenda kusukuma ipatikane pesa ya kujenga nyumba za walimu na kuhakihisha Shule hizo zinakuwana Michepuo ya Kilimo.
Akitoa pongezi kwa Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katibu Mkuu wa CCm amesema Serikali ya Mama Samia imefanya mambo makubwa ambapo imejenga Shule zaid ya 200 kwa kutumia fedha za Sequip hapa nchini.
Vile vile amewapongeza wananchi kwa kuanziasha mradi huo kwa kutumia nguvu kazi yao yenye thamani Zaidi ya Shilingi Milioni 17 na kuwataka wananchi wajiongeze kuzifanya Shule hizo kuongezewa madarasa ya kidato cha tano na sita.
Pia amezitaka taasisi zote za umma kabla ya kuanzishwa kwake utaratibu wa kuwa na hati Miliki za maeneo hayo ufanyika haraka ili kukwepa kesi na Migogoro ianayoweza kujitokeza hapo mbeleni.
Aidha amependekeza Shule hiyo ijulikane kwa jina la SHULE YA SEKONDARI MANOFU kwa kuwa mmiliki na aliyetoa ardhi yake kwa ridhaa ya kujenga Shule hiyo anaitwa Manofu ikiwa ni sehemu ya kuenzi na kuthamini mchango wa mwananchi huo mwenye uzalendo wa dhati katika Nchi yake.
Akiwa katika Shina namba 3 la Chama Cha Mapinduzi (CCM) lililopo katika kijiji cha Kwasemwariko kata ya Kilulu Wilayani Muheza Chongolo ameahidi kutoa mipira 2 mmoja wa wanawake na mwingine wa wanaume ikiwa ni sehemu ya kuwahimiza kujishughulisha na michezo kwa kuwa michezo ni afya, michezo ni biashara na huongeza uchumi na kuwataka waachane na mchezo wa bao ambao hauwasaidii kuongeza kipato.
Aidha katika Ziara yake yote amehamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la Sensa ya watu na makazi ili kuisaidia Serikali kupanga mipango yake ya maendeleo,
“Niwaombe ndugu zangu mjitokeze tarehe 23/8/2022 kuna sense ya watu na Makazi msipojitokeza mtashindwa kuletewa maendeleo stahiki katika Wilaya yenu, Sensa haina dini, haina siasa wala kabila huu ni mpango wa Serikali wa kutambua idadi ya watu wake ili iweze kuleta maendeleo, itasaidia kuleta dawa, kuongeza vituo vya afya ; mkihesabiwa vizuri kila mtu katika eneo lake atapangiwa mipango yake tujitokeze kuhesabiwa alisema Chongolo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.