Mwakilishi wa Kampuni ya Cotex iliopo Dar es salaam Frances Mfikwa jana tarehe 28/4/2020 amekabidhi matenki 2 ya maji kwa Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mwanasha Rajab Tumbo ili kuondokana tatizo la Upungufu wa Maji kwenye maeneo yenye Mikusanyiko.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Frances amesema lengo la kutoa msaada wa matenki hayo yenye ujazo wa lita 225 ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na Ugonjwa wa Corona (COVID-19) ambapo vifaa hivyo vitatumika kuhifadhia maji ya kunawa mikono katika maeneo hayo.
Nae Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo ameishukuru Kampuni ya COTEX kwa ushirikiano na Upendo waliouonesha katika kutambua jitihada za Serikali na kusaidia katika kutatua changamoto za Ugonjwa huu Wilayani humo.
Akiyataja maeneo yatakayopelekewa matenki hayo, Mhe, Mwanasha amesema tenki moja litapelekwa katika kituo kikubwa cha mabasi kilichopo katika kata ya GENGE na lingine litawekwa katika eneo la Soko kuu la Muheza Mjini lililopa katika kata ya Tanganyika ili kuepukana na changamoto ya Maji katika maeneo hayo.
“Tunashukuru kwa kutuletea matenki haya na sisi kama Serikali tunaendelea kuelimisha jamii kuchukua tahadhari za kuweza kutokomeza Corona.” alisema Mhe, Tumbo.
|
|
|
Katibu Tawala Wilaya Muheza Desderia Haule ( aliyebeba mkoba) akishuhudia makabidhiano ya Tenki kati ya Mwakilishi wa Kampuni ya COTEX Frances Mfikwa (kushoto) na Mkuu wa Wilaya Muheza Mwanasha Tumbo mwenye Hijabu. | Mwakilishi wa Kampuni ya COTEX Frances Mfikwa (kulia) akizungumza wakati wa makabidhiano ya Tenki yaliyofanyika eneo la Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri jana tarehe 28/04/2020. | Mwakilishi wa kampuni ya COTEX Frances Mfikwa (aliyevaa shati jeupe) akishusha Tenki kwa ajili ya makabidhiano |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.