Kamati ya kudumu ya bunge ya Ardhi, Maliasili na utalii ikiongozwa na Waziri wa Ardhi , nyumba na maendeleo ya makazi mhe, William Lukuvi ilitemelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba 10 za gharama nafuu uliopo katika eneo la charter kijiji cha Kibanda kata ya Kilulu jana tarehe 18\3\2018 ili kujiridhisha na ujenzi wa mradi huo.
Akizungumza katika ziara hiyo lukuvi amesema anailipongeza shirika la nyumba la taifa (NHC ) kwa kazi nzuri ya ujenzi wa nyumba 10 za gharama nafuu ambao mpaka sasa uko katika hatua ya umaliziaji ikiwa kiasi cha TZS milioni 135 kimetumika , Aidha ameiagiza Halmashauri kumalizia kulipa kiasi cha fedha kilichobaki ili majengo yaweze kukamilika uweze ipasvyo.
Kwa upande mwingine, Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Ardhi , maliasili na utalii wamesema wameridhia ujenzi huo kwani umefuata mkataba uliofanyika kati ya Hamashauri na Shirika la nyumba pia umefuata kanuni na taratibu za majengo ya Serikali.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo Mkurug.enzi wa Shirika la nyumba Bw Maulidi Banyani amesema mradi uliopo ni wa nyumba 20 za gharama nafuu ambapo nyumba 10 zinatekelezwa na Halmashauri ya wilaya na nyumba 10 za Shirika la nyumba ambazo mpaka sasa nyumba 10 za watumishi ziko katika hatua ya umaliziaji ikiwa 5 zina vyumba 3, sebule, choo na stoo ikiwa 5 zilizo salia zina vyumba 2 sebule , choo na stoo. Kwa upande wa nyumba za watumishi ziko katika hatua ya umaliziaji na zile za shirika zipo katika hatua ya Msingi .
Amesema mpaka sasa wamepokea kiasi cha Shilingi milioni 135 ikiwa kama sehemu ya mkataba pia wameweka marumaru ambayo haikuwa sehemu ya mkataba , ambapo kiasi cha fedha mpaka kukamilisha jengo ni TZS 390,306,600= hivyo basi wanadai kiasi cha TZS 255306600 Aidha ameitaka Halmashauri kukamilisha kiasi hicho ili wakamilishe kazi hiyo.
kamati ya bunge ikikagua nyumba za gharama nafuu za watumishi
|
|
Lukuvi akitoa maelekezo mbalimbali ya kiserikali
|
---|---|---|
|
||
|
||
Kamati ya bunge la kudumu ya Ardhi , maliasili na utalii ikikagua nyumba za gharama nafuu za watumishi zilizojengwa katika eneo la chatur kijiji cha kibanda kata ya kilulu jana tarehe 18\3\2019.
|
|
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe, William Lukuvi akitoa maagizo ya serikali jana katika mradi wa ujenzi wa nyumba nafuu unaotekelezwa katika eneo la chatur kijiji cha Kibanda kata ya Kilulu.
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.