Kamati ya fedha uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga imefanya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kipindi cha robo ya Kwanza 2022/2023.
Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo ya Madiwani na Wataalam ni Ujenzi wa Shule ya Sekondari Mpya ya Chatur ya kidato cha kwanza hadi cha sita iliopo katika Kijiji cha Kibanda kata ya Kilulu, Nyumba kumi (10) za Watumishi ambazo zimejengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo kijiji cha Kibanda kata ya Kilulu, Ujenzi wa Zahanati ya Kwakopwe na Kituo cha Afya Kwafungo ambacho kinajengwa kwa fedha za tozo za Miamala ya simu kiasi cha Shilingi Milioni 500 (500,000,000) ambapo mpaka sasa huduma za wagonjwa wa Nje zinatolewa katika Kituo hicho na wateja Zaidi 400 wamepata matibabu kituoni hapo.
Awali Mwenyekiti wa Kamati hiyo Erasto Mhina amepongeza juhudi ambazo zimefanywa na viongozi na wataalam katika kusimamia Miradi hiyo ambayo imelenga kuwasaidia Wananchi katika kupata huduma mbalimbali kama dhamira ya Mhe, Rais Samia Suluhu Hassan.
Nae Mwenyekiti wa huduma za Jamii wa Halmashauri hiyo amabaye ni mjumbe kwenye kamati ya fedha Mosses Siwa amewaomba Wataalam na kamati ambazo zinahusika kusimamia ujenzi wa Mradi wa Shule ya Sekondari Chatur na Kituo cha Afya cha Kwafungo kueleza ukweli kamati hiyo changamoto ambazo zinasababisha Miradi hiyo kutokukamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma.
Aidha Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Muheza Simoni Leng’ese licha ya kupongeza juhudi ambazo zimefanywa katika kusimamia Miradi hiyo amewaomba wataalam na Madiwani kuendelea kushirikiana katika kutekeleza Ilani ya Mwaka 2020/2025 ambayo imeahidi kusogeza huduma karibu kwa wananchi chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Kwa Upande wa Diwani wa Kwafungo na Mtendaji wa kata hiyo wametoa ushauri wao kwa kamati hiyo kwamba ili kuleta ufanisi kwenye miradi lazima Halmashauri iwe na wataalam wa kusimamia wakitolea mfano sehemu ya kuhifadhia vifaa (storekeeper) kwani kwa sasa shughuli hizo zimekuwa zikifanywa na watendaji au watumishi kada tofauti ambao hawana uelewa juu ya masuala ya manunuzi na Ujenzi.
Mwenyekiti wa Halmashauri akizungumza |
|
wajumbe wa kamati ya fedha |
|
|
|||
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mhe. Erasto Mhina akizungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya fedha, Uongozi na
Mipango mara baada ya kukagua mradi wa Shule ya Sekondari Chatur. |
|
Wajumbe wa kamati ya fedha wakijadiliana jambo mara baada ya kukagua miradi |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.