Mapema jana Tarehe 30 2025, Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Fedha pamoja na wajumbe wa kamati hiyo walifanya ziara ya ukaguzi wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa Wilayani hapo walitembelea jumla ya Miradi 5 katika Kata 4,ikiwemo miradi mitatu ya elimu,mmoja wa Afya pamoja na ujenzi wa Jengo la Utawala.Kamati ilikagua Shule mpya Shikizi Kijiji cha Misufini Kata ya Magoroto ambayo inajengwa kwa ufadhili wa Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Muheza na Naibu Waziri wa Habari,Sanaa,Tamaduni na Michezo Mheshimiwa Hamisi Mwinjuma pamoja na Benki ya CRDB Muheza.
Pia Kamati ya Fedha katika ziara hiyo wamepongeza Ujenzi wa Shule ya Sekondari Mhamba iliyopo Kijiji cha Bwitini Kata ya Mhamba inayojengwa kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa SEQUIP kwa kiasi cha Sh584,280,029 ambayo ipo hatua ya umaliziaji na Shule ya Sekondari kwa Bastola iliyopo Kijiji cha kwa Bastola Kata ya Makole kwa kuleta matumaini makubwa na kusema kuwa Miradi hii itatoa adha ya uhaba wa Shule katika Wilaya ya Muheza.
Aidha katika sekta ya Afya kiasi cha Shilingi milioni470 imetengwa kwa ajili ya kuendeleza Ujenzi na ununuzi wa vifaa katika Hospitali ya Wilaya ya Samia Suluhu iliyopo kata ya Lusanga ambapo Tsh.300milioni kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa tiba kwa ajili ya Mazoezi[Physiotherapy]na Sh170Milioni kwa ajili ya Umaliziaji wa Ujenzi wa Jengo la Kuhifadhia Maiti,Wodi 4, mbili za Upasuaji na Mbili za Magonjwa ya ndani za wanawake na wanaume pamoja na kukamilisha Mfumo wa Maji taka Jengo la Utawala.
Aidha Wajumbe wa Kamati wa Fedha na Mipango walipata wasaa wa kutembelea Ujenzi wa Jengo la Utawala lililopo Kijiji cha Tanganyika Kata ya Lusanga ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni3.3 zimetengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo hilo ambapo Wajumbe wa Kamati wamesisitiza kuwa Wafanyakazi waongezwe ili kuharakisha Ujenzi huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Muheza Mh Erasto Mhina ametoa pongezi na shukurani kwa Serikali ya awamu ya sitakwa juhudi kubwa ya kuboresha sekta ya Elimu na Afya na amewataka wakandarasi wa majengo hayo kuongeza kasi ya ujenzi wa majengo hayo ili kuleta manufaa kwa jamii
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.