Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe, Atashasta Justus Nditiye (mb) ameitaka jamii kutumia vizuri mawasiliano kwa kuwa ni chombo pekee kinachoweza kuleta tija katika maendeleo.
Amesema mawasiliano yakitumiwa vizuri husaidia kuleta mahusiano mazuri katika biashara hatimaye kuongeza kipato cha kaya na hatimaye mafanikio kupatikan katika jamii husika.
Ameyasema hayo wakati akizindua Mnara wa Simu wa TTCL uliopo katika kijiji cha Misalai kata ya Misalai Wilayani Muheza ambapo mnara huu utasaidia kurahisisha mawasiliano kwa wakazi wa kata ya Misalai na vijiji vya Jirani,
Vile vile ametoa miezi 3 kwa Kampuni ya TTCL kuboresha huduma ya mtandao walioweka badala ya 2G waweke Mtandao wa 3G utakaowawezesha wakazi hao kufurahia huduma za mitandao ya kijamii ili kuweza kuwasiliana na Ndugu zao waliopo nje ya Nchi.
Pia amewasihi watumiaji wa mitandao ya kijamii kutopotosha jamii katika masuala mbalimbali wala kupiga picha mbaya ikithibitika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
“Ni marufuku kupotosha jamii kwa namna yoyote ile , wala kupiga picha za uchi na kuziweka kwenye mitandao tukikugundua tutakuchulia hatua za kisheria alisema Mhe Nditiye”
Akizungumzia suala la utengenezaji wa barabara ya Amani –Muheza naibu Waziri amesema Mkandarasi amepatikana na ameshaaanza kutekeleza mradi huu ambapo kilomita 7 zitajengwa hali itakayopelekea wakulima na wafanyabiashara kupeleka mazao yao sokoni.
“Nawaombeni muwe wavumilivu suala la ujenzi wa barabara haljasimama tunasubiri hali ya hewa ikae vizuri ndio tuendelee kukamilisha ujenzi huu, ifahamike kuwa utengenezaji wa barabara ni kazi ya muda mrefu tumeanza na kilomita 7 kisha tutamalizia maeneo mengine , tunasubiri Mvua zipungue ndio tuendelee na utengenezaji” alisema Naibu Waziri.
Nae Mbunge wa Jimbo la Muheza Mhe Adadi Rajabu amepongeza jitihada za TTCL kujenga Mnara katika kata ya Misalai ameendelea kusisitiza kampuni kupanua wigo wa Mawasilaino katika kata zote 6 za tarafa ya Amani kuhakikisha zinakuwa na mawasiliano ya uhakika .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mwanasha Rajabu Tumbo amewataka wakulima wa mazao ya viungo kwenda kuuza mazao yao katika kiwanda cha kukausha mazao ya viungo kilichopo katika kata ya Lusanga iliokuwa (ofisi ya kata Lusanga).
Akitoa pongezi kwa Serikali awamu ya 5 inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli Diwani kata ya Misalai Mhe, David Bughe amesema anaishukuru Serikali hii kwa kuhakikisha inawapatia huduma ya mawasiliano hali itakayopelekea kuchagiza uchumi wa wama Misalai na tarafa ya Amani kwa ujumla kwani hapo awali mawasiliano yalikuwa yanapatikana kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni baada ya hapo maasiliano yanakata.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.