Jamii imetakiwa kujiepusha na vitendo hatarishi vya ngono ya jinsia moja(wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao), biashara ya ngono kwa wanawake, na matumizi ya madawa ya kulevya yanayofanywa na baadhi ya vijana ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU).
Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani iliyofanyika jana tarehe 1/12/2020 katika kitongoji cha Majengo ( majengo Shimoni ) kata ya Majengo Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Muheza ambaye ni Afisa tarafa Muheza Ndugu JAPHET NDAGAMUSU ameitaka jamii iwajibike kila mmoja katika kupambana na virusi vya ukimwi kwa kuepukana na ngono zembe isiyozingatia matumizi sahihi ya uvaaji mipira ya condom.
Vile vile amewata baadhi ya watu kuepukana na mila na desturi ambazo zimepitwa na wakati ambazo ni kurithi wajane, ndoa za utotoni kwa wasichana na mimba kwa umri mdogo kwani ni miongoni mwa sababu zinazopelekea ongezeko wa Ugonjwa huu.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa WilayaMuheza Flora Kessy amewaasa vijana kabla ya kuanza mahusiano mapya wafike katika vituo vya kutolea huduma za afya wapime afya zao ili waweze kuwa na taarifa sahihi za afya za wenza wao.
Awali akisoma risala ya siku ya maadhimisho ya Ukimwi duniani kwa kurejea kauli mbiu ya mwaka 2020 isemayo “Mshikamano wa kimataifa, Tuwajibike kwa pamoja’’Mratibu wa Ukimwi Wilaya Muheza Herieth Nyangasa amesema lengo la maadhimisho hayo ni kujumuika kwa pamoja kuwajibika kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi(VVU) kadhalika na kuwakumbuka ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza maisha kutokana na Ukimwi.
Akitoa taarifa ya takwimu za hali ya maambukizi ya Ukimwi Wilayani Muheza kwa kipindi cha kuanzia mwezi januari hadi Desemba 2019 Bi Herieth amesema jumla ya watu wote waliopima ni 34,148 miongoni mwao wanaume ni 15,061 ikiwa ni sawa na asilimia 44 ambapo Wanawake walikuwa 19,087 sawa na asilimia 56.
Aliendelea kuwa matokeo ya upimaji yanaonyesha kuwa watu waliokutwa na maambukizi ya VVU ni 856 sawa na asilimia 2.5 kati yao wanaume ni 326 sawa na asilimia 1.0 na Wanawake ni 530 sawa na asilimia 1.5. kitakwimu inaonyesha kuwa kila mwezi watu wasiopungua 71 wanapata maambukizi mapya ambapo kila wiki watu 17 huambukizwa na watu 2 hupata maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.
Akizitaja sababu za ongezeko la maambukizi ya virusi vya ukimwi Mratibu wa ukimwi amesema ni kutokana na upimaji wa VVU kuelekezwa zaidi kwa watu wenye vigezo vya kupima ambao wako kwenye mazingira hatarishi ya kupata maambukizi kutokana na tabia hatarishi au mazingira wanayoishi kama vile wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao(MSM), wanawake wanaofanya biashara ya ngono,(FSW), wanawake wadogo (AGYW) na Wanaojidunga (PWUDs) amabao wengi wao ni vijana
Aliongeza makundi haya yasipofikiwa katika upimaji kutakuwa na uwezekano mkubwa kupata maambukizi mapya ya VVU na kuambukiza wengine kutokana na kutopata taarifa sahihi juu ya huduma za ushauri nasihi, tiba na matunzo.
“Vijana wengi wako hatarini kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwasasabu katika ukuaji wao unawafanya kujaribu mambo mapya ikiwa ni sambamba na vijana kujamiiana wakiwa hawana tarifa sahihi kuhusu mabadiliko ya miili yao, magonjwa ya ngono na kukosa msaada wa watu wazima hali hii husababisha vijana hasa wasichana kujikinga zaidi kupata mimba kuliko UKIMWI”alisema BI NYANGASA.
Katika hatua nyingine ameitaja mikakati ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo Wilayani Muheza ikiwa ni pamoja na kutoa elimu inayofanywa na Asasi zifuatazo AMREF, WORLD VISION, SWAAT, SHIDEFA, SADEF, MUHEZA HOSPICE CARE, BAKWATA , SHIVYAWATA, MKUTA, ZICOSAD, AWCYS, AFRIHOVIC na baraza la watu wanaoishi na VVU(KONGA).
|
|
|
|
|
|
|
|
MWAKILISHI WA MKUU WA WILAYA JAPHET NDAGAMUSU AKIZUNGUMZA WAKATI WA MAADHIMISHO YA UKIMWI | MGANGA MKUU WILAYA MUHEZA FLORA KESSY AKIZUNGUMZA KWENYE HAFLA HIYO | MRATIBU UKIMWI WILAYA HERIETH NYANGASA AKIZUNGUMZA WAKATI WA MAADHIMISHO |
|
|
|
|
|
|
|
|
|||||
|
|
|
|
|
|
||
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.