Jamii imetakiwa kuepukana na fikra potofu za uwezeshaji tiba kinga za ugonjwa wa minyoo, kichocho, na usubi ili kutokomeza ugonjwa wa minyoo, kichocho cha tumbo ambayo ni magonjwa yanawasumbua watoto waliopo katika umri wa kusoma na waliochini ya miaka mitano.
Kadhalika dawa za usubi hazitakiwi kuepukika na ili kuweza kujiepusha na ngozi kuwa na madoa doa, kuwa na vipelena upofu, ugonjwa huu husababishwa na inzi weusi wanaokaa katika mito inyokwenda kwa kasi sana.
Katika Wilaya ya Muheza ugonjwa huu unapatikana zaidi katika maeneo ya tarafa ya AMANI katika kata za Mbomole, Zirai, Amani, Misalai, kwezitu na pamoja na kata ya Misozwe na Potwe
Akiwasilisha taarifa ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika kikao cha kamati ya Afya ya Msingi kilichofanyika tarehe 25/3/2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Muheza mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele wilayani Muheza Julius mgeni amesema katika kipindi hiki Halmashauri ya Wilaya Muheza inatarajia kutoa dawa za minyoo kwa wanafunzi 44,000 na wananchi 199,500 wanatarajiwa kupewa dawa za usubi.
Alisema ofisi yake inatarajia kutoa wanataraajia kutoa kutoa dawa kinga za magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mnamo tarehe 30/3/2021 ambapo dawa za minyoo na kichocho zitatolewa shuleni na dawa za usubi zitagawia katika kaya ambapo wataalam waliopata mafunzo watapita majumbani.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe. Mwanasha Tumbo aliwapongeza watendaji hao kwa namna walivyoweza kutimiza wajibu wao mpaka kufikia hatua ya kutotoa tena dawa za matende na mabusha.
Aidha aliwataka wajumbe wa kamati ya afya ya msingi kila mmoja kwa nafasi yake akaelimishe dalili za magonjwa haya pamoja na madhara yatakayojitokeza iwapo mtu atashindwa kumeza dawa hizi ili waone umuhimu wa tiba kinga hizo.
“kwa kuwa ugonjwa huu husababishwa na mazingira machafu nawaagiza maafisa afya wa vijiji na kata kusimamia usafi katika maeneo yenu ili kupunguza magonjwa yanayoambukiza, tusirudi nyuma, tuhakikishe na huo usubi hatunyi dawa kabisa leo , mkurugenzi mimi nikitembea nikakuta uchafu mahali popote pale iwe karatasi au chochote kile nitawajibisha watumishi hawa” alisema Mhe Mwanasha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Nassib mmbagga alisema wanaandaa mikakati ya kuhakikisha wanafunzi na wananchi wanameza dawa hizo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.