Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe, Halima Abdallah Bulembo kwa kushirikiana na kampuni ya Makazi Solutions wamekabidhi Hati za Viwanja 124 kwa wananchi ambao wamekamilisha taratibu zote za malipo ya urasimishaji.
Hati hizo zimetolewa kwa wananchi wa maeneo ya Kilapula, Machemba, Mkanyageni, Ngomeni, Azimio, Kwemkabala,Masimbani, Masuguru, Mbaramo, Teule, na Michungwani ambao wamekamilisha malipo ya urasimishaji.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika siku ya alhamisi tarehe 3/3/2022 katika Uwanja wa Kilapula Mhe Bulembo amewataka wananchi kuendelea kulipia gharama za urasilishaji kwa kuwa zina faida kubwa katika jimii ikiwemo kutatua migogoro ya ardhi katika eneo husika
Aliendelea kuwa faida nyingine ya hati ni hutumika kama dhamana kwamba iwapo mtu unahitaji kukopa katika taasisi za kifedha au mahakani au kituo cha polisi husaidia kupatiwa huduma ya dhamana.
Aliongeza kuwa Hati husaidia kumtambulisha mmiliki wa kiwanja kisheria hivyo basi anakuwa na haki zote katika kiwanja hicho kwa mujibu wa sheria na hii itamsaidia kurejeshewa fidia pale ambapo serikali itahitaji kuchukua ardhi .
Pia alitoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia ya kupotosha jamii juu ya masuala mbalimbali ya ardhi waache mara moja kwa kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa kazi za utambuzi, upangaji, upimaji na urasimishaji makazi Afisa Mipango Miji Happiness Namponji amesema mpaka sasa jumla ya hati 829zipo katika hatua mbalimbali, 68 ziko ofisi ya Kamishna Mkoa kwa ajili taratibu za kusajiliwa ikiwa 336 zimekamilika kuandaliwa na wananchi wameitwa kwenda kuweka saini na ili ziruudishwe kwa kamishna na 425 ziko katika hatua za mwisho .
Akizitaja changamoto za zoezi la urasimishaji Happy amesema mwitikiomdogo wa wananch katika kulipia gharama za kuandaliwa hati imeisababishia Serikali kukosa mapato ambayo husaidia kuwaletea wanachi maendeleo.
|
|
|
|
||
|
||
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.