Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga imekabidhi Cherehani tatu (3) kwa kikundi cha Vijana cha WADEE kazi cha Kijiji cha Kisiwani kata ya Kisiwani kinachojishughulisha na Ushonaji ikiwa ni sehemu ya kuendeleza kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza baada ya kukabidhi Cherehani hizo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mhe. Erasto Jerome Mhina amabae alikuwa Mgeni rasmi kwenye tukio hilo ameipongeza Serikali awamu ya sita (6) inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuwawezesha kiuchumi Vijana .
Amesema kupitia vifaa hivyo vitakwenda kubadilisha maisha ya Vijana wa Kisiwani kwa kuweza kutambua fursa mbalimbali ambazo zinaweza kuwapatia fedha ikiwa ni mapenzi makubwa ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa Watanzania wakiwemo wa Muheza Kisiwani
Awali Kaimu afisa Maendeleo ya jamii ya Wilaya ya Muheza Hassan Mwinyimkuu akipokuwa akisoma taarifa amesema vifaa hivyo vimetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ajilia ya kugawa kwenye vikundi vinavyojishughulisha na ushonaji, Uchomeleaji na shughuli za Aluminium vilivyopo kwenye Halmashauri kama sehemu ya mchango wa kuviwezesha vikundi hivyo kujiajiri.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kisiwani Shabani Chewaja na Mwekahazina wa kikundi cha WADEE kwanza licha ya kuishukuru Serikali na Watendaji wamesema vifaa hivyo vitakwenda kubadilisha hali ya kiuchumi kwa Vijana wa kikundi cha Wadee kwanza kutumia vifaa hivyo kwa umahili ili waweze kuwa mfano kwa Vijana wengine kwenye jamii na lengo la Rais wa Tanzania litimie la kuhakikisha Vijana wanawezeshwa kiuchumi.
MWENYEKITI WA HALMASHAURI AKIKABIDHI CHEREHANI KWA WAJASIRIAMALI |
|
|
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mhe. Erasto Jerome Mhina (kushoto) akikabidhi Cherehani kwa kikundi cha Vijana WADEE kilichopo katika kata ya Kisiwani kinachojishughulisha na Ushonaji wa nguo. |
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.